MPENZI WANGU KANIAMBIA HANITAKI ILA BADO TUNAFANYA MAPENZI?

iddimakengo Instagram profile with posts and stories - Picuki.com
Kaka mimi naomba ushauri wako, niko kwenye mahusiano na huyu Kaka ni mwaka wa nne sasa. Mimi nampenda sana lakini tatizo nikuwa hanijali kabisa, yaani anaweza hata kukaa miezi minne bila kunipigia simu na akinitafuta ni kama anataka kufanya tendo la ndoa au anashida ya pesa, kaka najihisi kuchanganyikiwa kwaninampenda sana.
Mwezi uliopita nimemuuliza kwanini ananifanyia hivi ameniambia kuwa hanitaki na hanipendi niendelee na maisha yangu, lakini cha ajabu wiki iliyopita alinitafuta, tukafanya mapenzi ila nilipomuuliza kuhusu mahusiano yetu bado akaniambia hanitaki nikipata mtu niolewe tu, kaka mimi bado nampenda nishauri nifanye nini ili nayeye anipende?
JIBU LANGU; Kuna wakati mwingine wadogo zangu mnatakiwa kujiongeza tu na kujua kuwa hamtakiwi. Kutokupendwa na mwanaume si kwamba wewe ni mbaya au si kwamba labda yeye ana cha maana sana, hapana, ni kuwa wakati mwingine upepo unakua hauko upande wako au mambo yanabadilika. Kuna mambo mengine mwanaume akikuonyesha unatakiwa kujua kuwa huyu si mwanaume wako na wewe kuondoka.
Najua utaumia lakini hakuna namna, mahusiano kama yako unapaswa kujua kuwa, una machaguo mawili, kwanza ni kumuacha ili uumie leo na maisha yaendelee au usubiri baada ya miaka mitatu, umeshabeba mimba yake akuache ukiwa single mother. Najua wadada wanasema “Lakini kaka mimi nampenda!” Dada zangu, hata mimi napenda kuwa na Ndege yangu binafsi lakini hujaniona nimeng’ang’ania uwanja wandege nikisema napenda ndege kuwa ndiyo itakuja.
Ukweli ni kwamba kama inafikia hatua mwanaume anakuambia kuwa hakutaki basi jua kuwa hakutaki. Najua unajiuliza, bona nikienda kwake tunafanya mapenzi na anaonekana kufurahia. Dada yangu, wanaume akili za wanaume katika kufanya mapenzi hazina uhusiano kabisa na mapenzi yenyewe, akili zao zipo kwenye tendo la ndoa tu, bingine ni mbwembwe.
Kwamba mwanaume anaweza kufanya mapenzi na wewe kila siku na akafurahia wakati hakupendi, wakati mkiwa mbali na kitanda anakasirika na hataki kukuona. Hivyo kama mwanaume anakuambia hakupendi, anakufanyia vituko vyote kukuonyesha kuwa hakupendi basi hembu kubali kuwa hupendeki na endelea na maisha yako, umia, umia, umia na acha maisha yaendelee. La sivyo utang’ang’ania na kujipendekeza na bado kuachwa utaachwa.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA