Ni ngumu sana kuthaminiwa kutokana na vile ulivyo navyo;

 Ni ngumu sana kuthaminiwa kutokana na vile ulivyo navyo; lakini ni rahisi sana kuthaminiwa na kupewa nafasi kwenye mioyo ya watu kwa sababu ya vile unavyovitoa, na ukishaijua siri hii, basi jambo lililo bora kuliko yote sio kuwa tu na vitu; bali jambo lililo bora zaidi kuliko yote ni kutoa vitu; maana ni kheri kutoa kuliko kupokea.!=Matend20:35.

Watu huwa hawawakumbuki wanaopokea sana; bali watu huwa wanawakumbuka na kuwaadhimisha wale wanaotoa sana; kwahiyo ukishalijua hilo haupaswi kukaa mkao wa kupokea sana; bali unapaswa kukaa mkao wa kutoa sana.!
Hakuna mtu aliyewahi kuweka alama kwenye hii dunia kwa sababu alikuwa mpokeaji sana; lakini watu wote ambao waliowahi kuweka alama kwenye maisha ya watu walikuwa ni watoaji sana wa vile walivyokuwa Navyo.!
Hakuna Mtu aliyewahi kuhesabiwa kuwa amebarikiwa kwa sababu ya vile alivyovipokea tu; bali kuna ambao wamedumu wakiwa wanaitwa kuwa wao ni wabarikiwa kwa sababu ya vile wanavyovitoa.!
Aliye na vingi ni kama vile ni rahisi kudhani ya kuwa huwa anaongezewa; lakini ukweli ni kwamba anayeongezewa zaidi kuliko wote ni yule anayetoa zaidi; kwa sababu hiyo Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji na Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.!=Mith11:24-25.
Hakuna aliye na uhitaji mkubwa sana wa vitu kama Mtumiaji wa vitu na hakuna mtu aliye na utele wa vitu kwenye maisha yake kama mtoaji wa vitu; kwa sababu hiyo watumiaji siku zote ndio wahitaji wa siku zote na watoaji wa siku zote ndio watu wa utele siku zote.!
Mtu wa maana kwenye maisha sio yule anayewaza kupokea sana; bali Mtu wa maana siku zote ni yule anayewaza kutoa sana; kwani anayewaza sana kutoa atajua na namna ya kupata vya kutoa sana; lakini anayewaza sana kupokea hataweza kujisumbua hata kuwaza namna ya kutoa hata kile alichokipokea.!
Hautaongezewa zaidi kile ambacho hauna uwezo wa kukitoa zaidi; bali utaongezewa zaidi juu ya mengi uliyo nayo ambayo unaweza kuwa tayari hata kuyatoa zaidi; kwani apandacho Mtu ndicho atakachokuwa na uwezo wa kukivuna ikiwa ni kile kile au ikiwa kimeongezeka zaidi; lakinibkwa vyovyote vile ni kwamba apandae ni lazima atavuna tu.!
Wakati wowote uwao mzuri kwenye maisha huwa sio wakati wa kupokea; bali wakati mzuri kuliko wakati uwao wote kwenye maisha huwa ni wakati wa kutoa sana ikiwa ni sehemu ya kile ulichokipokea sana au ikiwa ni sehemu ya kile umefanikiwa kuwa nacho sana.!
Pata sana na utoe sana na kwa kufanya hivyo utapokea sana pia.!
Ni kweli hauwezi ukatoa kile usichokuwa nacho lakini pia hakuna ambaye hana uwezo wa kutoa kile alicho nacho na hakuna mtu ambaye hana kitu cha kutoa.!
Wahitaji sana ndio wale wanaopokea sana na hao ndio wahitaji wakubwa sana na wanaofanikiwa kuushinda uhitaji sana huwa ndio wale wanaotoa sana; kwa sababu hiyo ni kwamba kwa vyovyote ni labda uwe kwenye wahitaji sana ambao ndio wale wanaopokea sana pasipo hata kutoa au uwe kwenye watoaji sana ambao ndio wale wasiokuwa na uhitaji na ambao wameshaushinda kabisa uhitaji!
Pata sana na ondoa uhitaji wako kwa kutoa sana kwani kuhitaji sana hakuwezi kumfanya mtu atoe hata kile alicho nacho; bali kutoa sana huwa kunaondoa kabisa uhitaji.!
Kumbuka kuwa kanuni ya kupanda haiwezi kujipinga hata kwenye suala la kutaarajia mavuno kwani apandacho Mtu ndicho atakachovuna,kwa vyovyote vile uvunaji sana huwa unatokana sana na upandaji sana.!
Kipimo cha kupokea sana sio kipimo cha kupokea kwenyewe; bali kipimo cha kutoa sana ndicho kinachoamua hata kipimo cha kupokea pia; kwa sababu hiyo Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.!=Luk6:38.
Ukweli ni kwamba hapa duniani Hatutamkumbuka Mtu yeyote kwa sababu ya vile alivyokuwa anavipokea sana; bali Kwenye hii dunia Tutalazimika kumkumbuka mtu kwa sababu ya vile alivyovitoa; kwani Dorkasi hatumkumbuka kwa sababu ya vile alivyokuwa navyo bali Watu walimkumbuka kiasi cha kumtafuta Mtume Petro kwa sababu ya vile alivyovitoa.!
Una karama, basi itoe sana na kutokea hapo utaweza kupokea sana pia.!
Una hela au vitu,basi tafuta namna iliyo sahihi ya kuitoa au kuvitoa na kwa kufanya hivyo utapokea sana; kwani wapeni watu vitu nanyi mtapewa pia.!
Toa sana ulicho nacho na kutokea hapo utafanikiwa sana kupokea hata kile usichokuwa nacho.!=Mith11:24-25.
Ukikwepa kutoa sana utakuwa umefanikiwa kuukaribisha uhitaji sana, na ukihitaji sana hautakuja ufanikiwe hata kutoa sana; kwani kuna atawanyae lakini huongezewa zaidi na kuna azuiae isivyo haki lakini huelekea uhitaji mkubwa sana.!
KUMBUKA KUWA.
Ni ngumu sana kuthaminiwa kutokana na vile ulivyo navyo; lakini ni rahisi sana kuthaminiwa na kupewa nafasi kwenye mioyo ya watu kwa sababu ya vile unavyovitoa, na ukishaijua siri hii, basi jambo lililo bora kuliko yote sio kuwa tu na vitu; bali jambo lililo bora zaidi kuliko yote ni kutoa vitu; maana ni kheri kutoa kuliko kupokea.!=Matend20:35.
Toa sana ulicho nacho na kutokea hapo utapokea sana hata kile usichokuwa nacho; kwani kuzuia sana huwa kunaleta uhitaji mkubwa sana.!
God bless You.!
Image may contain: 2 people, text that says "Artist Jafa"

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA