Licha ya kwamba ulimpenda kwa dhati, lakini yawezekana yeye aliona huwezi kumfikisha pale ambapo alitaka kufika.






 Licha ya kwamba ulimpenda kwa dhati, lakini yawezekana yeye aliona huwezi kumfikisha pale ambapo alitaka kufika. Na sio kwamba una mapungufu kiasi hicho au usingeweza kweli kumfikisha, hapana ila anadhani mapenzi ni miujiza.

Anadhani kila kitu kitatimia kwa wakati na labda pia anamhitaji mtu mkamilifu kwenye maisha yake. Mkamilifu yaani ambae hakosei japo ukweli ni kwamba mtu kama huyo hayupo.
Mwisho wa siku tamaa inamuongoza na sababu alishindwa kuona utu wako anakimbili vitu kama mwonekano, pesa, kazi nzuri, umaarufu akisahau kujua kama mwenye usafi wa moyo na anaye thamini mapenzi na kujua maana ya upendo ndo bora zaidi.
Usiogope, mwache aende! Huo sio mwisho wa maisha bali ndo mwanzo wa kuupata mwanga sahihi maishani na kuwa na mwelekeo hata pale utakapoanzisha mahusiano mapya.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA