SOMA NA SHARE UNAWEZA KUMSAIDIA DADA MMOJA HUKO!





Niwakumbushe tu Dada zangu kuishi na mwanaume bila ndoa hakumaanishi kuwa amekuoa hivyo zingatia mambo yafuatayo;
(1) Ddhana ya ndoa ni kuishi miaka miwili mfululizo chini ya paa moja na si kuishi miezi sita; kuna wale wanajidanganya kuwa mkiishi miezi 6 ni kama mmeoana, hapana, ni miaka miwili na mnapaswa kuishi sehemu moja. Sio kwamba mwanaume anaishi mwanza na wewe unashi kagera ukasema kuna dhana ya ndoa hapana.
(2) Mnapoishi muda mrefu dhana ya ndoa ni katika kugawana mali tu, lakini mwanaume anaweza kwend akuoa mwanamke mwingine na akakuacha, huwezi kuweka pingamizi kwakua tu mlikua mnaishi kama mke na mume, sanasana utadai mali ambazo mmechuma pamoja tu.
(3) Mali mlizochuma pamoja ambazo mtagawana nusu kwa nusu ni zile tu zenye majina yenu wote. Mali zenye majina yake ni zake hata kama ulichangia, ila unaweza kuthibitisha mahakamani kuwa na wewe ulichangia kiasi flani, iwe ni moja kwa moja kwa kutoa pesa au kwa kuwa Mama wa nyumbani kumtimizia makumu kama mume, utagaiwa kutokana na kile ulichochangia au kipimo cha kuwa Mama wa nyumbani na si nusu kwa nusu.
(4) Kutoa mahari inaweza kutambulika kama ndoa ya kimila na ukiwa na mwanasheria mzuri unaweza kuitetea hiyo lakini wengi wanakosea kwani baada tu ya kufunga ndoa ya kimila inatakiwa kusajili ndoa hiyo kwa Katibu Tarafa, kwa maana hiyo kuna ndoa nyingi za kimila zinaweza kupingwa mahakamani na zisiwe halali.
(5) Mali zenye majina ya watoto si mali zenu ni za mtoto hivyo huwezi kumfukuza mwenza wako katika hizo mali kwani ni za mwanae pia. Njia salama yua kubaki na mali zako ni kwa kuandika majina yako na kuwa na document pamoja na risiti zote kuonyesha kuwa mwenza wako hakuchangia. Ukinunua kiwanja kwa jina la mtoto, ukajenga mkaishi pamoja huwezu kumfukuza wala mkiachana hamuwezi gawana kwani ni mali ya mtoto ila itategemea kama umemuweka nani kama msimamizi.
SHARE KWANI KUNA DADA KAJISAHAU ANAITA MUME HUKO!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA