USIKUBALI KURUDISHA MOYO WAKO KWA MSALITI



Sio kila EX Wako anayeomba mrudiane anamaanisha, wengine huomba kurudi Ili wakutesti tu jinsi ulivyo dhaifu, Jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna misimamo wala future.
Mtu mmeachana miezi 6 iliyopita, leo anakutesti mrudiane, na wewe ulivyo mvivu wa kifikiri, upo upo tu, alafu unajikuta tena ukimpa fursa nyengine ya kuendelea kukuchezea. Ina maana miezi yote hiyo ulikuwa umeganda unasubiria mrudiane na yeye? Kurudia matapishi ya EX ukitegemea amebadilika ni sawa na kupika sufuria la makande kwa mshumaa, utaambulia masizi tu.
Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi tena? Nini kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi? Shtuka mtu wangu usije ukawa kipezeo au jamvi la wageni.
KUWA NA MSIMAMO ukisema Its Over umaanishe, Sio unakuwa na hisia zinazopepea kama bendera ya katibu kata wa kishumundu. Mtu kama hakukuelewa tangu mwanzo achana nae, siku akijirudisha mwambie haupo kwaajiri ya majaribio ya kisayansj
Usiendelee kutoa sifa mbaya kwenye mapenzi et "siku hizi hakuna mapenzi ya dhati" wakati wewe ndio hukuwa makini juu ya mapenzi yako.
Huwezi kusoma degree ya law aalafu U-Apply kazi ya Chief Accountant wa bodi ya tumbak. Kila siku utasingizia balance sheet haina jurisprudence. Lawyersl
Mmenielewa. Acha kudate watu wasiojielewa, Usidate kwa sababu uko Lonely, usiwe desperate kuingia mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Kunduchi Beach.
Ingia kwenye mahusiano pale moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na veins, auricles, na aorta za oyo Wako kwamba He/She Is Really The One.
Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui, ukimuuliza anataka Kuwa wapi ndani ya miaka 5 Ijayo anakwambia Mungu anajua dont Worry, halafu BBM na Instagram unajiita Baby ake mie Iam in Love.
Kuwa makini utaishia kutumika na kufua Boxer hadi..........
Date The Right Person,With Right Reasons, In A Right Time Uone Kama Mapenzi Hayapo
Chukua hiyo then fanyia kazi.
SHARE KAMA UMEIPENDA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA