FANYA HAYA KULINDA MAHUSIANO YAKO ILI MUWEZE KUDUMU.
Katika maongezi huwa tunaongea mambo mengi sana yahusuyo maisha, michezo, mahusiano, siasa, kazi nakadhalika. Ili uwe muongeaji mzuri na mchangamfu kwa watu unaoongea nao ni busara kuchunga kauli zako na kujua unaongea nini kwa mtu/watu wanaokusikiliza.
Watu unaoongea nao watavutiwa na kuendelea kukusikiliza iwapo watapenda unachokiongea. Kwa upande mwingine kuongea na watu kunaweza kukujengea uhusiano mzuri au kubomoa uhusiano wenu. Kufahamu ni mambo gani watu hawapendi kusikia kutakusaidia kujua nini cha kusema na kipi usiseme.
Haya ni mambo ambayo wanaume na wanawake hawapendi kusikia kuhusu wao
Wanaume hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao
1. Kumwambia kuwa hawezi kutunza pesa vizuri au ni mfujaji mali.
2.Kumwambia yeye hana akili au ni mjinga.
3. Kumwambia yeye ni mfupi (andunje)
4. Kumwambia yeye si mcheshi au amezubaa sana.
5.Kumwamba anaonekana kama amezeeka.
6. Kumwambia yeye ni mwoga, dhaifu au ni mshamba wa mambo.
7. Kumwambia yeye hajui kujali au kumbembeleza mwanawake.
8. Kumwambia yeye hana hela au ni maskini.
9. Kumwambia yeye ni bahili sana.
10. Kumwambia kuwa yeye hajui kuongea na watu vizuri. (domo zege)
Pia usithubutu kumlinganisha yeye na wanaume wenzake waliomzidi kimaendeleo au kwa chochote kile.
Kama wewe ni mwanamke na unataka kuimarisha au kukuza ujuzi wako wa kuongea na wanaume kuwa makini sana unapotumia maneno hayo kuzungumza na wanaume kwani wengi wao hawapendi kabisa kusikia wakiambiwa hivyo.
Wanawake hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao
1. Kumwambia yeye hana umbo la kuvutia au ana kasoro na umbile lake.
2. Kumwambia yeye ni mnene sana au ameongezeka uzito.
3. Kumwambia kuwa yeye amezeeka.
4. Usithubu kumtajia umri wake kuwa yeye ni mkubwa sana.
5. Usithubutu kumuuliza alishawahi kuolewa hapo nyuma.
6. Usimfananishe yeye na mwanawake mwingine ambaye hapendezwi naye.
7. Kumwambia kuwa hajapendeza na nguo alizovaa.
8. Kumwambia kuwa yeye ana sauti mbaya isiyo nyororo ya kuvutia.
9.Kumuuliza yeye ana watoto wangapi ikiwa maongezi yenu hayahusu mambo ya kifamilia.
10. Kumlinganisha yeye na mwanamke mwingine ambaye amemzidi kwa kitu chochote.
Mfano: Uzuri, Pesa, Mali n.k
Natumaini kuwa utakuwa umejua mambo ambayo watu hawapendi kusikia , huchukia kila wanapoambiwa mambo hayo kuhusu wao. Kila mtu hupenda kusifiwa kwa namna yake ya kipekee, hivyo chunga usimfadhaishe mtu kwa kumzungumzia vibaya .
Mpe mtu sifa nzuri na stahiki kuhusu yeye na kwa pamoja mfurahie maisha kwakuwa kila mtu ana uzuri na kasoro zake!
#TuiyalindeMahusianoYETU2016
❤❤❤❤❤