KAMA NI KUCHEPUKA CHEPUKA BASI KAMA WENGINE ACHA KUJIFANYA MTAKATIFU KUMBE UMEJAA LAANA!




Ni muda mrefu sana nilikua nataka kuiandika hii mada sema nasahau ila jana nimepoke simu moja ikanikumbusha niiandike. Kuna wanawake wengi katika ndoa na hata katika mahusiano ambao hulalamika kua waume zao wanachepuka, wana wanawake wengine lakini pia hutumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii wakichat na wanawake wengine. Baadhi utawasikia wakisema “Mume wangu utakuta kutwa nzima yuko online anachat lakini mimi nikimtumia meseji hajibu!”

Wanawake hawa utakuta wanaambiana vumilia, piga goti usali, muombe Mungu, funga kwaajili ya ndoa yako. Wanafunga kweli, wanasali kweli na kumuomba Mungu lakini mambo hayabaidliki. Sasa wakati mwingine ni Mungu hajaamua lakini wakati mwingine ni laana ya yale ambayo huwafanyia wanawake wengine. Twende sasa, mumeo akiwa na tabia kama hizi moja kwa moja utakua mpweke, utakua mwenyewe, huna mtu wa kuchata naye kwani marafiki zako wameolewa wako na mahusiano yao na wana furaha.

Unakutana na mwanaume huko mtaani anakuambia ameoa, lakini si mwanaume wa mtaani ni rafiki yako, mfanyakazi mwenzako ambaye ni mume wa mtu. Wanawake wengi wa namna hii wanakuaga na rafiki mmoja wa kiume wa kumuambia matatizo yao, huyu huwasikiliza, huwajali, hupiga simu na hata kuwahudumia, kwakifupi anawafariji. Tena wengi wa namna hii wanakua wameoa au wana wachumba siriasi na huyu mke wa mtu anajua. Lakini cha ajabu kwakua mumewe anchelewa basi nayeye atachata na huyu mwanaume mpaka usiku wa manane.

Watatumiana meseji, watasifiana na wakati mwingine kutoana out kuondoa upweke, hawachepuki na wala hawafanyi kitu kibaya kwa mujibu wao lakini huyu mwanamke ambaye ndoa yake imemshinda anasahau kua huyu mwanaume anayechat naye, anayetoka naye out anayemuambia matatizo yake, naye ana mke, mpenzi. Anashindwa kuelewa kua mke wa yule mtu naye akiona meseji zake hatajua kama ni marafiki tu atajua kama ni mchepuko na anaibiwa.


iddimakengo #part2 #anziapostiliyopita

Maumivu yake ni yaleyale, lakini wakati yeye analalamika mumewe yuko online lakini hchat naye yeye nayeye yuko online anachata na mume wa mtu au mchumba wa mtu, akilalamika mumewe kila muda yuko na simu anaboa lakini yeye anakua na simu anachat na mume au mchumba wa mtu. Yale yote ambayo analalmika kua mumewe anamfanyia anafanya na mume au mpenzi wa mtu. Iko hivi kama umeolewa na ndoa yako imekushinda ukaenda kutafuta faraja kwa mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu au ana mtu wake siriasi basi jua unaharibu ndoa na mahusiano ya mtu mwingine.

Jua kua unatengeneza maumivu kwa mwanamke mwingine! Kwa maana hiyo unapopiga magoti na kumlaani anayeharibu ndoa yako ni kama unajilaani kwakua unafanya kitu kilekile. Sio kwaba ukiacha kufanya huyo mwanaume ataacha kuchat na wanawake wengine hapana, ni mshenzi tu, wewe unamuona kua ni mwanaume mwema na wakati mwingine unawaza “Kwanini mume wangu asinmgekua anajali hivi?” Ukweli nikua mke wake naye analalamika kama wewe kwani mumewe anaendekeza wanawake wengine ambao ni wewe kama mumeo.

Lakini ninachosema hapa acha kumuumiza mwanamke mwenzako kwakua ndoa yako ishakushinda. Ila kama ukiona huwezi basi chepuka basi kama wanawake wengine tukujue ni mshenzi na Malaya tu kama wengine kuliko kujifanya mtakatifu na kujiliza liza mpaka unatoa makamasi ili uonekane mwema kumbe wewe ni wale wale tu unaharibu ndoa za watu! Unajitafutia tu laana, hata kama kweli umpweke ndiyo uchukue mume wa mtu kuchat naye, wako kakushinda unataka wa mtu! Acha ujinga huo, acha kujitafutia laana, kamaunachepuka chepuka tujue moja lakini si kujishaua kua “Hakuna kitu kinachoendelea tuanchata tu ni marafiki!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA