NILIVYOKARIBIA KUJIUA BAADA YA KUMFUMANIA MUME WANGU NA MDOGO WANGU WA DAMU!




Haikua mara yangu ya kwanza mimi kumfumania mume wangu, lakini hata siku moja sikuwahi kufikiria kama anaweza kutembea na mdogo wangu wa damu, tumbo moja tena toka nitoke. Alishatembea na marafiki zangu, akatembea na wafanyakazi wenzangu, mabinti wa kazi na majirani zangu lakini sikuwahi kufikiria kama anaweza kutembea na mdogo wangu.

Nakumbuka ilikua ni siku ya Alhamisi, nilikua nimetoka Kariakoo kusagulasagula vinguo kwaajili ya kutembeza mtaani. Hii ilikua ni baada ya kuacha kazi mwaka mmoja kabla, si kwa kupenda kwangu, nilikua na kazi nzuri, nilikua na mshahara mzuri lakini kwa ujinga wangu niliacha mara baada ya mwanaume kuniambia kuwa kama sitaacha kazi basi ananiacha.

Kila mara nilipokua nikimfumania aliniambia simtoshelezi kwani niko bize na kazi ndiyo maana anachepuka. Kwa ujinga wangu nilimkubalia nikaacha kazi kwa makubaliano ya kuwa atanifungulia biashara ili nisiwe bize niwe na wakati wa familia. Lakini baada ya kuacha kazi, aliponiona kuwa sina kipato ilikua ni kama nimefungulia mlango wa manyanyaso.

Alizidisha kulala nnje, akawa hatoi tena pesa za matumizi na wakati mwingine pamoja na kuwa ni mtu mwenye cheo chake lakini watoto walikua wakishindia uji na alikua hajali. Baaada ya kuona kua hahudumii familia na kuona hana mpango wa kunifungulia biashara niliamua kutumia mtaji kidogo niliokua nao nikaanza kununua nguo za mitumba na kutembeza mtaani kama mmachinga. Kutoka katika maisha ya kiyoyozi mshahara zaidi ya milioni mbili kwa mwezi nilirudi kuuza mitumba.

Najua mtashangaa kwamba kama nilikua napata pesa yote hiyo kwanini sikua na akiba, ukweli nikuwa mimi ndiyo nilikua kila kitu katika familia, nikimhudumia mume, nikihudumia watoto, nilisomesha ndugu zangu, nikisomesha wadogo zake, nikisomesha wanangu na kila kitu, hata kuwekeza ilikua mimi. Pesa za mume wangu zilikua zikiishia katika wanawake wengine na kunywa pombe, yeye alikua ni mtu wa marafiki na hakujali kabisa kuhusu ndugu wengine

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA