FAIDA ZA MBEGU ZA MLONGE KATIKA UZAZI

 


Mlonge ni mti maarufu sana Duniani kote hata hapa kwetu Tanzania husussani mkoa w Kigoma. Wao hutumia kama dawa ya kuteguka, maumivu ya mwili au miguu, tumbo na hutumika zaidi kwa matumizi ya kivuli. Ziko aina nyingi za mti wa Mlonge, lakini zinazofahamika sana ni zile aina saba za mlonge zilizo maarufu kati ya 13 zilizopo ; Mlonge Drouhardi – Madagascar Mlonge Longituba – Ethiopia Mlonge Ovalifolia – Angola na Namibia Mlonge Concanensis – Inayostawi zaidi India na katika nchi za Afrika Kaskazini. Moring Stenopetala – Inayostawi zaidi katika nchi za Ethiopia na kaskazini mwa Kenya Moringa Peregrina – Inayostawi zaidi Sudani, Misri, Syria (Peninsula) Uarabuni na Kaskazini mwa bahari ya Shamu. Mti wa Mlonge hutibu Magonjwa mengi sana yanayomsumbua binadamu na baadhi ya Magonjwa hayo ni kama ifuatavyo :- Kisukari Ugumba Tatizo la Figo Tatizo la Moyo kuwa mkubwa Kupata maumivi unapokutana na Mwanamke/Mwanaume Mapele sehemu za siri Tatizo la Miguu na Magoti Maumivu ya mikono Mishipa ya ngiri Madonda ya koo Meno Vibarango Vidonda ndugu degedege Madonda ya Tumbo Mgongo Kiuno Matatizo ya nguvu za kiume na kike 

JINSI YA KUTENGENEZA DAWA YA MLONGE NA MATUMIZI YAKE 

1). KWA UGONJWA WA KISUKARI Menya tunda la mbegu na uchukue mbegu tatu za Mlonge kisha zitafune mbegu hizo tatu kutwa mara tatu 1 x 3, pia hakikisha unakula mbegu hizo baada ya kula na kushiba. Halafu chukua mizizi na magome mabichi ya mlonge, chemsha kwa pamoja baada ya kuzitwanga dawa hizi na kuzisafisha kisha epua na kunywa glasi moja ikiwa bado dawa ina uvuguvugu, tumia kutwa mara tatu kwa siku saba. Nenda Kacheki Hospitali na upumzike kwa siku mbili. Baada ya hapo chukua miziz ya mlonge kausha na utwange, saga iwe kama unga. Kila siku asubuhi jaza kijiko kidogo cha chai na uweke kwenye maji moto na kunywa kama chai kikombe kimoja asubuhi kabla ya (kuswaki) kupiga mswaki. Tumia dawa hii kwa muda wa siku kumi na nne yaani wiki mbili. 

2).UGUMBA NA UZAZI Chukua mbegu za mlonge kisha zitafune tatu, pia kiasi fulani zina ukakasi – ugwadu, kwa hiyo inatakiwa usijali ukakasi wake, wewe tumia tu. Kama kawaida tumia tatu kutwa mara tatu na bila kusahau uzitumie baada ya kula chakula na kushiba. Chemsha mizizi pamoja na magome baada ya kutwanga na kulainika, ikichemka tumia glasi moja kutwa mara tatu kwa muda wa wiki moja. Chukua maua ya Mlonge yaliyokauka kisha yaweke kwenye chujio la chai, unaweka maji ya moto juu ya chujio hiyo na unajaza kikombe cha chai unakunywa kama chai. Hii husaidia kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba. Tumia dawa hii hadi utakapopata mafanikio ya kuwa mjamzito. Hakikisha unapotumia dawa hii uwe unakutana na mumeo, usitumie kama hauna hakika ya kukutana na mumeo kimwili. 3). MAUMIVU UNAPOKUTANA NA MUME Chemsha mizizi, magome na majani, maji yake safisha sehemu za siri kwa muda wa siku saba.

 4). HARUFU MBAYA MDOMONI, KWAPANI NA MWILI MZIMA Tafuna mbegu tatu kutwa mara tatu, sukutua mdomo kwa kutumia mti wa mlonge, pia oga maji yaliyochemshwa kwa magome na mizizi ya mti wa Mlonge. Chukua mizizi na magome safisha kisha chemsha tumia kwa kunywa kikombe kutwa mara tatu 1 x 3 Saga mbegu za Mlonge tia ndani ya uji, maji vuguvugu au maziwa 1 x 1 tumia dawa hizi kwa pamoja. 

5). UPELE SEHEMU ZA SIRI – FANGASI Tafuna mbegu tatu kutwa mara tatu na pia chukua mizizi, magome na majani mabichi ya mti wa Mlonge. Tumia kupaka au kuosha na maji hayo sehemu zinazowasha na zile zillizoathirika pakaa asubuhi na jioni kila baada ya kuoga.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA