Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Ahisi Wewe Ni Mwanaume Wa Ndoto Yake

 


Ushawahi kupatikana katika hii hali?

Umeona demu mzuri ukaamua kumuapproach.

Ukamtongoza kwa siku kadhaa na bila kusumbuka akakukubali.

Baada ya wiki au mwezi mambo yakajeuka akakukataa.

Ukaona labda haikuwa bahati yako so ukatongoza demu mwengine mrembo.

Naye akakukubali lakini baada ya wiki akakukataa.

Mtindo ukawa ni huo huo, kila ukitongoza demu baada ya masiku au wiki anakukataa bila sababu za wewe kuelewa.

Je, kuna tatizo? Je mbinu unazozitumia kuapproach mwanamke kama huyu hazifai ama unacheza gemu yako vibaya.

Katika ukurasa wetu wa Facebook kuna msomaji wa N.M Blog alikuwa na wasiwasi wa kuwa anawatongoza mademu wazuri lakini anashindwa kuwamudu. Hivi ndivyo alivyotutumia ujumbe wake:

 Hello Nesi Mapenzi. Mimi nina bahati ya mademu  beautiful lakini penzi langu na wao hudumu muda mfupu sana. Inafikia mahali huwa natoswa na wananikataa. So nifanyeje? Naomba ushauri [imehakikiwa]    -Naseeb

Ok, jambo la kwanza ni kuwa nampongeza Naseeb kwa kuwa ana uwezo wa kutongoza mademu warembo bila wasiwasi wowote.

Pili ni kuwa nampongoza kuwa kuachwa na mwanamke si jambo ambalo linamsumbua akilini mwake, kawaida wakati unapotongoza mwanamke huwa kuna asilimia 50 ya kukubaliwa na asilimia 50 ya kukataliwa so kuweka matumaini yote kwa mwanamke ni jambo lisilofaa kabisa.



Tofauti na dhana ya wanaume wengi wanaofikiria, kudumu na mwanamke baada ya kumtongoza ni jambo rahisi sana. Hii inaweza kufanikishwa kirahisi iwapo utafuata mbinu ambazo ni za uhakika na dhabiti. Na kwa kueleza mbinu hizi hapa Nesi Mapenzi tumekuja na mbinu nne kuu ambazo ukizitumia ipasavyo utamfanya mwanamke aone kana kwamba ulikuwa mpenzi wake tangu jadi.

Zama nami!

Hatua za kumfanya mwanamke ahisi umekuwa ndotoni mwake tangu jadi


Hatua hizi ambazo tutazieleza zinaambatana na mbinu ya MMWILIKO. Hii hufanya kazi vyema kwa kuwa utakuwa unatuma ishara za kisiri kwa mwanamke kwa akili yake bila yeye kutambua. Unaweza kumwilika vitu hivi vinne.

1. Mwendo wake  wa kupumua
Mbinu hii ni kuiga vile ambavyo anapumua. Kama mwanamke unayemzimia na unatoka naye deti unataka akuone kana kwamba ulikuwa wake tangu kitambo, anza kuiga vile ambavyo anapumua. Kama kawaida yake anapumua kwa uzito basi pia wewe iga vile vile anavyopumua.

2. Toni ya sauti yake
Hii ni mbinu ambayo wengi huifanya bila wao kutambua...kuiga toni ya sauti ya anayempenda. Ukitaka kujua kama mwanamke amekupenda angalia vile jinsi ambavyo anavyoongea. Ukiona kama kuna toni flani ya sauti ameiga kutoka kwako basi ni ishara ya upendo. Hivyo hivyo, ukitaka mwanamke akupende na akuone kama anastahili kuwa nawe milele basi iga toni yake ya sauti. Kwa mfano kama anapenda kuongea kwa toni ya juu unaweza kuanza kuiiga sauti hio wakati ambapo munaongea issue ama swala muhimu. Hapa atakuchukulia na umakini zaidi tofauti na wakati ambapo unaongea kikawaida.

3. Mwendo wake wa kuzungumza
Tofauti na toni, mwendo wa kuzungumza ni vile ambavyo anatamka maneno kwa kasi flani. Kama umeshawahi kugundua ni kuwa kuna baadhi ya wanawake wanaopenda kuongea kwa haraka. Na pindi unapoongea nao kwa haraka wanajiskia huru kuongea na wewe zaidi na zaidi. Mbinu hii unaweza kuitumia kwa mwanamke unayemzimia. Kama anaongea pole pole wewe iga mwenendo huo na kama atakuwa anaongea kwa kasi vivyo hivyo iga. Bila yeye kujitambua ataanza kujivuta kwako kwani atahisi kana kwamba kuna kitu ambacho mnagawa pamoja lakini hatoelewa ni kitu gani hicho.

4. Miondoko yake ya mwili
Miondoko yake ya mwili inaweza kuwa mambo yote ya jumla anayopenda kufanya kwa kutumia mwili wake ambayo anaitambua na kuifahamu anapoifanya au la. Mfano anaweza kuwa anapenda kupesa macho yake mara kwa mara, kushika vidole vyake, miondoko yake ya mdomo, sura nk. Ukianza kuiga mbinu moja wapo anayoipenda kuifanya basi itafikia mahali flani atahisi kana kwamba kuna kitu ambacho mnafanana nacho.

Hakikisha kuwa wakati ambapo unafanikisha mbinu hizi mwanamke aina hii hapaswi kamwe kuelewa ya kuwa unamwilika matendo yake. Hii inapaswa ifanikishwe kifioa ili asipate kufahamu kama unafanya hivyo.

Mbinu hii ukiifanikisha ipasavyo basi utamfanya mwanamke ajihisi huru na wewe zaidi na aone kama amekufahamu kwa muda mrefu.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA