KWANINI USIRUDIE UHUSIANO/NDOA ILIYOKWISHA UMIZA MOYO WAKO UKAAMUA KUACHANA NAE

Wahenga na misemo yao;-



Huwezi kuzoa maji yakimwagika, vivyo hivyo huwezi kurudisha UPENDO ULIOKUFA kwani Mapenzi IMANI na mpaka uone umeshindwa maana yake IMANI imekwisha, Maana yake kama MAHUSIANO ama NDOA ikishindwa kufikia malengo ya awali na wawili hao kuachana, Halafu baadaye mmoja akabaini kwamba NI MHITAJI WAKO huku hapo mwanzo alikubari kuondoka Basi kaa ukijua jambo hili;-

Kwa maana hiyo anagundua wewe ulikuwa muhimu na kwa wakati sahihi uliweza kuwa BORA kwa Moyo na mwili wake.
Kwanini usikubari kurudi kwa Mtu uliye achana nae;-

Mtu anajaribu kuona kama baada ya yeye kuondoka je ulipata wa kumzidi na akibaini hakuna niamini ATAKUPA JAKA LA MOYO kuliko hata mwanzo, Japo sio wote ila kama mwanzo ulishindikana kwanini awamu ya pili iwezekane

Hilo swali kaa nalo jiulize mara kwa mara itakusaidia, Maana kama PENZI LILIBUMA MWANZO haliwezi kupata ukombozi kwa NAFASI nyingine

Kukubari aende maana yake ni kuijua THAMANI yako, na akiomba kurudi na ukakubari hapo ni wewe kuwa HUNA UJANJA
