JINSI UNAVYOWEZA KUEPUKA KUVUNJA NDOA/MAHUSIANO YAKO




Ni jambo la kawaida kwa wana ndoa kuwa na siku mbaya, ni jambo la kawaida kwa mtu kuchoka, umetoka kazini na umeudhiwa, kuna rafiki zako wamekuudhi au kukufanyia kitu kikubwa ambacho kimekuathiri sana. Una mawazo sana na wakati mwingine unatafuta mtu wa kumtolea hasira zako, aliyekuudhi labda ni Bosi wako au Mama yako na huwezi hata kumjibu, unarudi nyumbani au unakutana na mpenzi wako unaona kuwa yeye ndiyo mtu sahihi kumtolea hasira zako.

Unamjibu vibaya, kumtukana au hata kumpiga! Anakuuliza kitu badala ya kumjibu kama anavyostahili au kutumia busara na kumuambia kuwa hauko vizuri basi wewe unapaniki, unafanya hivyo ili angalau akujibu umshushie hasira zote. Kama unataka kuwa mtu wa furaha basi hembu epuka hiki kitu, mwenza wako hastahili kushushiwa hasira kwakua wewe ulikua na siku mbaya. Kumbuka si yeye aliyeisababisha na kumbuka maneno yanaweza kukutoka au ukafanya kitu kibaya ambacho hakiwezi kufutika tena.

Halikua kosa lake kwamba Bosi wako ni kichomi, si kosa lake kwamba mashoga zako wanakusimanga, si kosa lake kuwa Mama yako anakusumbua na si kosa lake kuwa huna pesa. Jifunze kunyamaza zaidi unapokua na hasira, fikiri mara mbili kabla ya kuongea kwani wewe unaweza kusahau na kusingizia ulikua na mawazo, kusingizia kuna watu walikukwaza lakini yeye hatasahau kwani utakua ndiyo mtu umemkwaza, haikupunguzii chochote kumuambia mke/mume/mpenzi wako kuwa una mambo mengi kichwani hivyo akuache upumzike!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA