KUJIAMINISHA KWAMBA HAKUNA TATIZO HAKUONDOI TATIZO! JIFUNZE NAMNA YA KUTATUA MATATIZO YAKO


Moja ya somo kubwa ambalo wanawake wengi hufundishwa kila siku ni uvumilivu. Kila mwalimu wa ndoa ambaye utamsikia tukianza na Mama anapoongea na binti yake basi humuambia kuwa ndoa ni uvumilivu. Ni kweli ndoa ni uvumilivu, lakini kitu kikubwa ambacho watu wengi hushindwa kuwaambia wanawake wengi ni kuwa wanatakiwa kuvumilia nini?

Lakini pia hata wakiwaambia nini cha kuvumilia basi hushindwa kuwaambia ni kwanini wavumilie. Kwa mfano mkulima anapolima anakaa kuvumilia kipindi fulani ili apate mavuno, kama ni mahindi basi yaje mahindi na kama ni mtama uje mtama. Anavumilia akijua kuwa ni kwanini anavumilia, anajua kuwa mwisho wa siku atapata kitu fulani.

Lakini binti anayepigwa na mume wake anapoambiwa na Mama yake kuhusu kuvumilia kama akimuuliza Mama yake nivumilie nini sana sana ataambiwa hata Baba yako alikuwa ananipiga kama unavyopigwa lakini kama binti atahoji kidogo na kumuuliza ulipata nini baada ya kuvumilia, sana sana utasikia anasema si unaona mpaka sasa niko naye lakini hatakuambia kuwa mpaka sasa nina furaha!

Lakini kama ukichunguza kidogo utakuta huyo Mama bado anaendelea kupigwa au Baba kaacha lakini ni kwakuwa kachoka anamtegemea Mama hivyo inabidi awe mpole tu lakini Mama naye hakuna alichopata kwa kuvumilia. Ninachosema hapa ni kuwa, watu wengi hufundisha uvumilivu kana kwamba unaweza kutatua matatizo ya Ndoa.

Sana sana ni kuyaahirisha na kuyafungia macho kana kwamba hayapo. Kufumbia macho au kusema kuwa tatizo fulani halipo kamwe hakuwezi kuliondoa hilo tatizo, linaendelea kuwepo na mmoja kuumia. Ndiyo maana mimi nasema kuwa kama ukiona ndoa yako ina matatizo, badala ya kuvumilia basi hembu angalia namna ya kulitatua hilo tatizo.

Labda mapenzi yamepungua, mume kaanza kuchelewa kurudi nyumbani, hembu jiulize utafanyaje ili awahi, kama una kitabu changu basi soma sehemu ya tatu. Huna furaha, mume hakujali, umefanya kila kitu kumfurahisha, badala ya kuvumilia basi hembu jifunze namna ya kujitengenezea furaha yako mwenyewe na kama una Kitabu changu basi soma sehemu ya nne.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA