KWENYE MAGROUP MITANDAONI KUWA MAKINI UTAVUNJA NDOA YAKO!




Kua makini sana kwenye mambo unayojadili kwenye mitandao. Wanawake wana magroup mengi na wengi wanapenda kutoa siri zao za ndani kwakua tu Group limeandikwa “Wanawake Tu” basi wanatoa kila kitu, tena vingine vyakudhalilisha wanaume zao. Kabla ya kutoa siri zako kwenye mitandao huko unakoamini mume wako hajaona basi kumbuka mabo yafuatayo.

(1) Kuna watu wanakujua na wanamjua mume wako, unaweza usijali lakini vuta picha unacomment mwanaume wako ni Kibamia au haendi dakika mbili, halafu kuna wafanyakazi wenzake, kuna watu alisoma nao, kuna dada zake wanakujua unadhani watajisikia raha? Hivi mume wako akijua unamtangaza unadhani atakuchekea?

(2) Wanaume wanashika simu za wake zao; Wakwako anaweza kuwa hashiki simu yako, ila kila siku shoga yako si analalamika kuwa mume wake anakagua simu yake? Sasa unafikiri hasomi. Lakini watu wenye upendo hawafichani, kuna wakati mume na mke kuna umbea mnapiga, sasa mashoga zako waume zao wanaona kwanini umdhalilishe wakwako.

(3) Wanaume wengi wana akaunti feki majina na picha za kike wapo huko kwenye hayo magroup. Hii ni hasa kwa Facebook, kuna wanaume wengi hujiunga magroup ya wanawake, wakwako anaweza kuwa mmoja wapo au wa jirani na ukamtangaza.

UHSUURI WANGU; Kua makini na unachoandika, acha kutangaza madhaifu yako kwa watu ambao hata kukusaidia hawakusaidii. Wengi wanakua tu wanachangia mada kuwaponda waume zao. Kama ni lazima kuomba ushauri hembu tumia hata akaunti feki basi.

Au fanya hivi, wasiliana na Admin, hata kama yeye humuamini sana kwani na wengine ni wambea fanya hivi. Jitumie meseji screenshot mtumie kama umeombwa ushauri na mtu mwingine na si wewe. Kwamba labda kuna tatizo unataka kujua suluhu, uliza kana kwamba ni mtu mwingine kaomba ushauri na si wewe, NISHAMALIZA.

NB; Mabaharia achaneni na haya magroup mtajiua kwa presha bure. Hata kama unamfuatilia mke wako basi cha kuingia humo, ni mambo ya kike na kuna wakati watataniana kama wanaume tunavyotaniana mambo ya uongo utani ukachukulia siriasi nusu kuchanganyikiwa.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA