USIVUNJE UHUSIANO/NDOA YAKO KWA SABABU HUJAPATA SEX ULIOKUWA UNAITEGEMEA



Uliye naye ni zaidi ya anayekuja kwa sababu starehe ya KITANDANI ni kwa dakika tu lakini UPENDO ni wa kudumu maisha yote. Mapenzi ya zama hizi yamekuwa ni kama kupenda taarifa ya habari au matukio tu. Mtu mmoja atatamani taarifa kwa Gazeti, mwingine atatamani taarifa kupitia Instagram, mwingine Facebook na mwingine TV. Kuna wakati watu huhitaji taarifa kutoka kwa waandishi na vyombo tofauti vya habari lakini ujumbe wa taarifa ni ule ule. Katika uhalisia huu ndiyo maana upendo limekuwa jambo adhimu mno hata wengi wanajikuta wanawalilia watu kisa Mapenzi.

Hatari kubwa duniani ni kumpoteza Mtu aliye na dhamana moyoni mwako kisa tu hakupi raha unayoisikia kwa mashoga ama marafiki. Wakati unamuacha, ukweli ni kwamba ataumia sana, Pengine hata akaanza kutengeneza namna nzuri ya kujiponya, wakati huo wewe utakuwa umejipa tumaini na kujiaminisha kuwa uko na mtu anayejua kukukuna vilivyo huku ukiwa umepofuka kwa mahaba ya mpito. Amini usiamini leo hii kuwa hakuna mwanaume au mwanamke yeyote anayempenda Mke au Mume wa Mtu ni tamaa tu na ubinafsi ndivyo vinavyotawala.

Anayesaliti penzi ni fisadi wa mapenzi. Ametawaliwa na ubinafsi pamoja na tamaa na kwa lugha fupi ana hisia zembe. Madhaifu hata yawe makubwa kiasi gani kwenye mahusiano ama ndoa yako, wewe yabebe kama yalivya kwa sababu tayari umeingia penzini huna sababu ya kutoka kisa tu kuna mwingine amekwambia kuwa yeye anapata yale uliyohitaji awe nayo mwenzi wako. Siku zote ajaye ni mpya lakini ukimjua atakuwa zilipendwa.

Baki njia kuu ili hata kama ukipotea ni rahisi kupata msaada, Kuliko kupita njia ya mkato ambako kama likikupata ulilokuwa ukilitafuta utaishia kulalamika tu. Wengi wanapenda vilivyoundwa bila kumjali aliyeviunda tena akilini mwao wanasema kuwa "Aliyeundwa haijui thamani ya mhunzi" ila ufahamu kuanzia sasa kwamba, kwa sababu unataka kuonja ladha tofauti tofauti, hao wote pamoja na utamu wao kitandani watapita na kitu pekee ambacho hakitakuacha ni majuto.

Katika maisha ya mahusiano na ndoa, ukiamua kutafuta mpenzi mpya kisa uliye naye hakuridhishi kitandani au ana udhaifu fulani usiokufurahisha, UTAJUTA. Ukweli ni kwamba unakuwa hujamaaliza tatizo, ila tu unakuwa umeanzisha tatizo lingine.

AMUA KWA BUSARA

#LeoNaLuckson

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA