Mapenzi ya mbali, Acha kukusanya makosa unaboa ataacha kuongea na wewe

 Ni kama mchana ulikuwa na kazi moja ya kukusanya makosa yake. Unaongea na marafiki zake kujua nyendo zake na kujua huko aliko mchana wote alikuwa akifanya nini, unampigia kila mtu unayemjua, unakusanya ushahidi, kupitia ukurasa wake kuwa ka like wapi na wapi.

Kacomment nini na sehemu gani, alikuwa online muda gani na hakuwa akichati na wewe. Usiku ukipiga unajiandaa kumsuta, akikuambia siku yake labda kakudanganya kidogo au kadanganya sana unaaanza kumsomea makosa yake, mbona hivi  vile sijui vile.

Yaani badala ya kunyegeshana usiku basi ana kazi ya kujibu shutuma. Mtu kama huyu hatatamani kuongea na wewe tena, achana na mambo anayofanya huko hayakuhusu, labda kama unataka kumuacha lakini kama bado unampenda na kila siku ni kufuatilia hata kaenda chooni mara ngapi?

Utampoteza, unaboa na kila siku atajifanya bize kwani anajua huna cha kuongea. Lakini utamfanya na yeye kila siku nikutafuta ushahidi wa namna ya kujitetea kabla ya kuongea na wewe. Yaani anakua kama wakili anaenda kwenye kesi kila siku lazima atafute ushahidi wa kujitetea. Badilika utampoteza!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA