Namna ya kukwepa kumfanya MWANAUME wako kuwa mtu wa kukunyanyasa na kukudhalilisha!

Kama unachekelea kila anapowadhalilisha na kuwadharau rafiki zako/ watu wengine, unaona kawaida tu na huongei chochote. Ndiyo anaanza na rafiki yako, mara ooh mbaya, mara anasura ya ajabu, mara kakaa kimasikini masikini, mara kisauti chake cha ajabu, mara mshambamshama, yaani kila saa atatafuta sababu ya kuwakosoa marafiki zako.

Kuwadhalilisha mbele yako na mbele za watu wengine. Sasa uanachekelea kwakua ni marafiki tu, bila kujua kua unamjenga na kumruhusu akutukane na wewe, awatukane ndugu zako na tabia nyingine za namna hiyo. Wakati mwingine hata unakubaliana na yeye unachangia na unachombeza pale anapowadhalilisha na kutukana maumbile yao!

Sasa kama una mpenzi ana tabia za namna hiyo mbadilishe mapema, ajue hutaki yeye kudhalilisha watu wengine kwani ukimuacha nakuambia akimaliza marafiki atahamia kwa ndugu zako kisha kwako. Kwamba huo kwake kudhalilisha watu ni kama ugongwa, usidhani kama wewe uko salama kwakua hakudhalilishi wewe kwa sasa, hapana hata wewe anafanya hivyo.

Muambie hapana sipendi unavyowaongelea marafiki zangu vibaya, sipendi unavyotukana watu bila sababu, onyesha huwezi kuvumilia na kama mlikaa sehemu ondoka na kasirika kabisa. Hapo utakua umempa ujumbe kuwa mimi siwezi vumilia mambo ya namna hii. Mwenyewe ataona kama huwezi kuvumilia rafiki yako akidhalilishwa basi huwezi kuvumilia Mama yako au ndugu yako na wewe huwezi kukubali udhalilishwe.

Mwanaume wa namna hii ni kama mtoto mdogo, ukimzoesha na kumchekea kudokoadokoa ipo siku ataiba. Nilazima ajue kuwa kitu anachoifanya hata kama hakufanyii wewe lakini kinakukera. Acha kujidanganya kuw ahakufanyii wewe, acha kujidnganya kua hayakuhusu, kumbuka hao marafiki anaowadhalilisha hataishi nao wewe ndiyo utakua ukiishi naye kila siku swali ni je utaweza kumvumilia?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA