DALILI 7 ZA MWANAUME ALIEMCHOKA MPENZI WAKE.


Wanawake ni itapendeza kama utaizingatia hii,ila kama haitakuwa na maana yote pia ni sawa pia.
Kwa kawaida jambo lolote lina kuwa na ishara Fulani kabla ya kutokea tukio husika,pia hata hivo hivo katika mapenzi,kuna dalili zake pia,nimekuandalia dalili chache za mwanaume ambaye ameanza kumchoka mpenzi wake.
Zama nami.......
Dalili ya 1
Mwanaume anaanza kuonyesha hasira na kuhamaki kwa kila unachokifanya hata kama ni kitu kidogo. Hii ni kwasababu penzi limempungua au kumuisha na hivyo anakosa uvumilivu kwako. Anaweza kukupayukia hata ukiwa katikati ya watu, hatojali unavyojisikia kwa yeye kufanya hivyo. Utashangaa na kujiuliza mbona mwanzoni aliweza kunivumilia? Jibu ni kwamba penzi limepoa au kuisha
Dalili ya 2
Kwa kawaida mwanaume anavyompenda mwanamke huwa na kiu ya kumfurahisha, hufanya vitu kuhakikisha mpenzi wake anatabasamu na anajisikia murua. Kila siku kiu ya mwanaume ni kuona mwanamke anatamani kuendelea kuwa ndani ya penzi hilo. Mapenzi yakiisha vitu hivi vyote vinapeperukia mbali.
Dalili ya 3
Mapenzi ya mwanaume yanapokwisha kwa mpenzi wake anakosa kabisa kuwa na muda naye. Mwanzoni mlikuwa mnakuwa na muda wa pamoja sasa hapati tena muda huo na kila ukiuliza visingizio kibao, mara kazi, ubize, mara safari, kuumwa au kuchoka n.k. Yaani inakuwa bora atumie muda wake akiwa na rafiki zake kuliko kuwa na wewe. Vicheko vya pamoja mkiwa peke yenu vyote vinakwisha. Ukiona hivyo jua hiyo taa nyekundu ndugu yangu.
Dalili ya 4
Dalili hii yaweza kufanana kidogo na niliyokwishaisema. Mwanaume anapoacha kumpenda mwanamke hupunguza sana au kuacha kabisa kumjali na kumhudumia mpenzi wake. Inakuwa ngumu kwake kukufanya ujisikie mwanamke au ujisikie aalumu kwake. Atawatendea wengine mema na kuwajali lakini si wewe. Zile bashasha na malavidavi aliyowahi kuwanayo hutoyaona.
Dalili ya 5
Mapenzi ya mwanaume yanapopungua au kuisha kwako utaona jinsi inavyokuwa ngumu kuwasiliana na wewe. Unapomwonyesha umuhimu au uhitaji wako wa mawasiliano yeye anaona mzigo mkubwa. Anakuwa mzito kuzungumza, mgumu kuzionyesha hisia zake kwako, mara nyingine inakuwia ngumu kugundua lini amefurahi na lini amekasirika. Zamani alikusikiliza, sikuhizi hakusikilizi tena. Zamani ulijua alipo na anachofanya sikuhizi ukiuliza unazua ugomvi.
Dalili ya 6
Mwanaume anapompenda mwanamke humruhusu mwanamke huyo kuyajua maisha yake yote. Maisha ya mwanaume huyu yanakuwa kama kitabu kilichowazi. Hafichi kitu wala kuishi maisha ya kona kona. Tofauti yake ni kwamba mapenzi yakimwisha utaona siri zinakuwa nyingi, haujui nini kinaendelea kwenye maisha yake na wala haoni umuhimu wa kukushirikisha kinachoendelea kinachomhusu yeye.
Dalili ya 7
Penzi la mwanaume linapoisha juu yako mara nyingi huwa anaona shida kukushirikisha kwenye maisha yake au yeye kushiriki maisha yako. Furaha yake inakuwa yake na yako inabaki kuwa yako wakati mwanzoni furaha ya kwako ilikuwa furaha yake. Ukifanikiwa kitu na yeye anajisikia furaha lakini si sasa. Inapofikia hapa utaona mnakaa nyumba moja kama wapangaji wawili na si mtu na mwenza wake.
Ukifanikiwa kuyaona hayo hupaswi kupanic na kukata tamaa mwishowe ukachukua maamuzi mabaya,ambayo yataathiri maisha yako kiujumla.
Wataalam Wa mambo wanasema kua kila jambo ni LA kupita tu, basi hata hilo pia LITAPITA tu...
May be an image of 1 person

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA