UMEKUBALI KUOLEWA KUBALI BASI KUACHANA NA NDUGU ZAKO, HUJAWACHOKA TU!

Utakuta mwanamke analilia kuolewa, anahangaika sana kuomba na kusali, kutegeshea Mimba na hata kutafuta Mganga ili tu aolewe.anabahatika kweli anaolewa, anakutana na mwanaume anampenda na yuko tayari kutengeneza maisha. Lakini sasa binti anakua kama amesahau kitu huko kwao, kwanza kila siku anapiga simu kwao.
Hii si mbaya kuwajulia hali, lakini itoshe tu uwajulie hali sio kila siku kumpa taarifa mume wako, mara Mama anakusalimia, Mama kasema hivi, Mama sijui vile, nilikua naongea na mdogo wangu, sijui kaenda shule, sijui nani kafanya hivi! Daaa mpaka inaboa, unaweza kuona kama kitu cha kwaida na inawezekana mume wako akakusikiliza kwakua anakupenda.
Lakini Dada yangu nikuambie tu unaboa, hakuna mwanaume ambaye anataka kusikia stori za kwenu kila siku, hata kama si matatizo, hata kama ni furaha lakini kama kila siku ukiongea na ndugu yako unamuambia mume wako basi jua kuwa kashachoka kusikia. Tena haiishii hapo, mwanaume ambaye anasikia hivyo kila siku anakua na wasiwasi.
Kwanza anawaza huyu kila siku anaongea na kwao kuna siri huku ndani kweli? Hata kama husemi chochote lakini yeye hajui hivyo anadhani kuwa unavyoongea ongea na ndugu zako unamuambia mambo yenu ya ndani. Pili anawaza hawa hawapangi kunitawala kweli, mbona kama maamuzi mengi ni ya Mama yake na ndugu zake.
Lakini pia mume anawaza hivi huyu ana akili zake au kila kitu mpaka aamuliwe na ndugu zake, anaona kwamba huko kuongea kila siku ndiyo kunakusaidia kuwaza na huna mawazo yako. Mwanaume wa namna hii hawezi kukuambia kitu cha maana kwani anajua utaenda kusema kwenu, hata mambo ya maendeleo anaweza asikushirikishe kwakua anaamini unapendelea ndugu zako zaidi!
Dada yangu umeshaolewa hembu waache ndugu zako wapumue. Sisemi usiwapigie simu ndugu zako, hapana unaweza kuwapigia hata kila dakika lakini hembu acha kumuambia mume wako. Mumeo hapaswi kujua kama unaongea nao kila saa, unamtia mashaka ya bure, kwani ukimuambia kasalimiwa na Mama yako ndiyo atanenepa?
Hembu jipe muda, unaweza kusema labda kila baada ya wiki ndiyo unamuambia niliongea na Mama anakusalimia. Muache apumue kusikia habari za ndugu zako, tena kwa wanaume wengi ukishaanza kuongea habari za ndugu zako, kuwasifia au kuongea tu kuwa wanaendeleaje anahisi unataka kumuomba pesa kutatua shida za kwenu!
Lakini ubaya pia hata kama kwenu wako vizuri wana hela ile kumuambia tu ni kama kumringishia kuwa kwenu wako vizuri na mbaya zaidi ni kama unamuambia mumeo kuwa huridhiki na maisha anayokupa na unawakumbuka ndugu zako. Nisikuchoshe nimalizie tu kusema wanaume hatutaki kusikia mambo ya kwenu kila siku hata sisi tunayetu!
KAMA MAKALA HII IMEKUBARIKI BASI HEMBU #SHARE NA WENGINE
May be an image of 2 people and people standing

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA