AMRI 10 ZA UCHUMBA UTAOFIKA MBALI.


1.Usizini. Tendo la ndoa ni kwa waliopo kwenye ndoa ndio maana likaitwa tendo la ndoa sio tendo la uchumba. Ukiona mchumba analitaka ujue hana mpango na ndoa! Geuza mabehewa kabla hajakuzinisha.

2.Usikope mkopo kusomesha mchumba hilo ni jukumu la wazazi wake, au kununua kiwanja pamoja, kujenga nyumba pamoja na mchumba  n.k hasa kama unadhani kwamba utaumia iwapo uchumba ukivunjika. Yafanye iwapo unaamini hayatakuumiza hata uchumba ukivunjika, na wala huna mpango wa kudai urudishiwe chochote. Katika hili Wengi wamelia mno!.

3.Acha kujiaminisha sana kwamba utamuoa au atakuoa kwani uchumba sio ndoa, uchumba ni uchumba tu na utabaki kuwa uchumba  na lolote laweza kutokea kama si upande wako basi upande wake. Wale yaliyowakuta wananielewa vizuri hapa.! Kwahiyo uwekage na ka balansi ili ukipigwa za uso usizile kuoa au kuolewa milele. 

4.Usiweke agano na mchumba, maandiko yanatambua agano la ndoa sio agano la uchumba. Katika uchumba unaweza kuweka ahadi lakini usiweke Agano. Mfano: kujiapiza eti mimi nisipokuoa kamwe sintaoa tena maishani mwangu au nisipoelewa na wewe kamwe sintaolewa tena.. Haya maagano yameghalimu wengi. Acha mapenzi ya Mungu yasimame katika uchumba wenu badala ya viapo na maagano. Kumbuka unaweza kufungwa kwa maneno ya kinywa chako ukafa bachela!

5.Usizae na mchumba ili akuoe. Hili linatokea sana kwa wadada ambao hawajaokoka. Ama kwa kudanganywa "nizalie kwanza ndipo nitakuoa" au wao wenyewe kujitegesha apate mimba akidhani ndo atapendwa zaidi. Binti yangu nakupa amri hii wengi wamezalishwa na wakatelekezwa, kama na wewe unataka kutest haya endelea. Ila usije kwangu unalia baadaye.! Maana nitakupuliza makofi kwanza kabla ya kukushauri lolote. Ebo! (Just kiding)

6.Msichukuane kienyeji enyeji. Ndoa inataratibu zake, na taratibu hizo zinaambatana na baraka zake ambazo kamwe hutazipata usipofata utaratibu uliowekwa na Mungu na pia na jamii yako. Shela lina raha yake asikwambie mtu dada! Sasa wewe unabebwa usiku kama mtu anaiba kuku vile? Unajiaibisha, unaaibisha ukoo, unaaibisha jamii na kabila lako, unamwaibisha Mungu na nafsi yako. Kama mnapendana sio lazima harusi njooni madhabahuni tuwaombee baada ya ibada mkaanze maisha ya ndoa. Tena na hii corona arusi hamzidi watu 6 wali apo si nusu kilo tu? Unakwama wapi?

7.Usioe au kuolewa na mtu kwa kumhurumia.

Ni kweli kaonesha upendo, ni kweli anakujali n.k lakini swali kuu la kujiuliza ni je huyo mtu yumo moyoni mwako? yaani unampenda? Umeridhika naye au unajikokota kwakuwa umekosa unayemtaka? na kwakua anakusaidia sana misaada? Ndoa nzuri ni ile ya watu wanaopendana sio ya upendo wa upande mmoja. Utakuja kujikuta umo ndani ya ndoa na mtu ambaye huna hisia naye kabisa ni kama uliingia kwenye ndoa kulipa fadhila au mkopo.

8.Uchumba usiwe siri kali. Utakuja kujikuta umeolewa na mume wa mtu au umeoa mke wa mtu. Kama nyote wawili mnastahili kwanini kuficha ficha sana mahusiano yenu utadhani ni dawa za kulevya? Yaani uchumba unafikisha miaka 3 wazazi hawajui, pasta wako hajui, ndugu hata mmoja hajui, matokeo yake unaharibikiwa wakati ungesaidika mapema kama ungliweka wazi. Mpendwa ukiona mchumba wako hataki watu wajue anakuchumbia huenda kuna kitu anakuficha, chunguza. Hata matapeli hapa mjini wakitaka kukuibia huwa wanakuvuta pembeni au wanakunyima nafsi ya kushirikisha mtu wa pili..ishu isije kubumbulika.Namfaham mtu fulani aliyeoa mara ya pili akimtelekeza mkewe kijijini na watoto. 

Jichunge usiwe mke wa pili bi mdogo bila kujiandaa! Kuna majamaa hayako serious na maisha ati!

9.Usioe au Usiolewe na mtu aliye kuwa na ndoa ikavunjika bila kujua ukweli wa sababu za ndoa ile kuvunjika.  Na hapa ili kupata sababu za kweli uliza toka vyanzo vingine vya habari sio kwa huyo mhusika hatasema ukweli zaidi ya kujitetea na kuonesha alivyokuwa hana hatia. Nijuavyo mimi huwa inahitajika bidii toka mume na kwa mke ili ndoa idumu. Vivyo hivyo hata kuvunjika lazima wote washirikiane kuivunja.  Sasa wewe weka mbele tamaa yako ya kuolewa, unajidai hutaki kujua yaliyopita subiri yakukute!

10. Usiolewe na mtu asiye mcha Mungu. Na dalili ya mtu kumcha Mungu ni kusali/kuabudu. Mtu asiye abudu  hampendi Mungu. Huo ndio ukweli. Sasa kama mtu hajui kumpenda Mungu aliyemuumba na anayempa uhai kila leo atajua kukupenda wewe? Mtu kama ameshafarakana na Mungu wewe ndio utawezana naye?  Unajua mtu akishabanwa na hamu ya ndoa haya mambo huwa wanayapuuza lakini wakishapata pata joto ya jiwe, ndipo wanakumbukaga but too late!


AMRI 10 ZA UCHUMBA HADI NDOA....
1. Hakikisha mahusiano yako na MUNGU hayaharibiwi. Mungu hawezi kukupa mtu atakayekutoa katika uwepo wake. Mpenzi sahihi ATAKUSOGEZA karibu zaidi na MUNGU.
2. Usikae kwenye mahusiano ambayo hayana MIPANGO: angalau baada ya miezi 6 ya mahusiano ni lazima zile hatau za mwanzo zianze, kama kumjulisha kiongozi wa kiroho na wazazi/walezi. Pia ujue mnatarajia lini kufunga ndoa. (UNDATED PLAN IS NOT A PLAN).
3. Hakikisha AMEKOMAA: Ndoa ni kwa ajili ya wanaume na wanawake; siyo kwa ajili ya wavulana na watoto wa kike. (Marriage is for MEN not for BOYS).
4. Usiolewe au kuoa kwa ajili ya MALI, ELIMU, PESA, AU NAFASI ya mtu huyo unaye-husiana nae.
5. Usioe au kuolewa kwa sababu ya presha za watu… “unaoa lini? au unaolewa lini?”. Subiri muda wako Mungu akuletee mtu sahihi.
6. Usifanye tendo la NDOA wakati wa UCHUMBA…. Ni “TENDO LA NDOA”…. Siyo “TENDO LA UCHUMBA.” Kama hana subira, basi fanyeni haraka mfunge ndoa.
7. Usioe au kuolewa kwa sababu UNA MWONEA HURUMA muhusika…. Labda amekufatilia sana sasa unaona hatia kutomkubali. Hakikisha kuna mapenzi ya dhati.
8. Jihadhari kufanya MRADI WA PAMOJA (mambo ya fedha, kununua kiwanja, shamba, nyumba) na MCHUMBA kabla ya kuwa na uhakika 100% kwamba mtaoana. Hata mkiamua kufanya mradi wa pamoja, kila mmoja aweke pesa yake hadi mtakapoana. Huwa inaleta shida kubwa na maumivu endapo uchumba utavunjika. (SIYO VIBAYA LAKINI KUWA MAKINI SANA).
9. Usichukue MKOPO kwa ajili ya kuandaa SHEREHE YA ARUSI. Fanya sherehe inayolingana na uwezo wako.
10. Mtegemee MUNGU katika kila hatua ya mahusiano yenu…. UCHUMBA hadi NDOA.
NB: Kitabu chetu kiitwacho "AMRI 10 ZA UCHUMBA" kitatoka hivi karibu.
-
May be an image of 3 people and footwear

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA