KIJANA UNAINGIA KWENYE NDOA; HAKIKISHA MWANAMKE ANAKUJA KWAKO SIO UENDE KWAKE




Najua kuna mazingira mengine ambayo yanamlazimisha mwanaume unapooa kuhamia kwa mwanamke. Labda umeoa wakati huna kazi (ingawa sikushauri hivyo) uko kwenye mchakato wa kuoa kazi ikaisha, au umeoa Mwanamke ambaye ana watoto na alishatengeneza familia yake. Lakini kwa kijana ambaye ndiyo unaingia kwenye ndoa kitu cha kwanza ni kuhakikisha kuwa mwanamke nakuja kwako.
Hata kama ana nyumba yake, hata kama shemu anayoishi ndiyo nzuri zaidi, hata kama ana uwezo mkubwa wa kifedha, lakini sehemu ya kuishi inapaswa kutafutwa na mwanaume, wewe ndiyo ulipe kodi, useme hapa ni kwangu. Kama ni kijana, unaoa mwanamke ana nyumba ni vyema ukamuambia Mama nyumba yako pangisha ila njoo tuishi hapa nyumba ya kupanga. Isipokua labda kama ana watoto au hakuna namna nyingine ya wewe kuweza kupangisha.
Hii ni kwasababu wanaume tunanyanyasika mapema, hata kama mwanamke hakunyanyasi anakupenda, lakini ukichelewa kurudi akakuambia kwangu hunirudii saa nane utaona anakunyanyasa kwakua ni kwake kumbe ni kawaida kwa wanaume kuambiwa hivyo hata wale wenye nyumba zao. Lakini kitu kingine ni kuwa wanawake wanachoka mapema, ukimfuata kwake ile ladha ya kuolewa inaondoka na ni rahisi kuanza visirani hivyo mwanamke anapaswa kuja kwako sio uende kwake.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA