MY STORY; MUME WANGU SIKO VIZURI NJOO TU UNIONE HATA KAMA HUTANIPELEKA HOSPITALINI!




Hakuna mtu nilikua namchukia kama mke wangu, nilikua namuona ni kisirani, mwanzo wakati ndoa inaanza tulikua tuko vizuri, lakini baada tu ya kupata ujauzito alianza kelele, alikuas ni mtu wa kulalamikia kila kitu. Kwanza alikua analalamikia marafiki zangu, alikua ananiambia kuwa wananiharibu kwakua walikua ni watu wa starehe sana, ni kweli kila sikui kwao ilikua ni pombe tu, maisha yalikua ni kufurahia.
Mimi niliona kama ananibana na kutaka kunipangia maisha. Pili ilikua ni ndugu zangu, mimi kwetu ndiyo nilikua na uwezo kuliko wengine hivyo shida kidogo wanakimbilia kwangu, hata dada zangu waliokua wameolewa walikua wanakuja kwangu. Hali hiyo ilimkera sana mke wangu, mara nyingi alipenda kuniambia, unaona wenzako wanafanya mambo ya maendeleo lakini shida wanakuja kwako.
“Dada yako na mume wake anajenga, lakini eti hawana hela ya ada kulipia mtoto wanakuja kwako. Mume wangu ukoje, kwanini wasiache kujenga na kusomesha watoto wao kwanza, wewe kiwanja kishakua msitu hutaki kujenga. Tulikua tunagombana sana, ndugu zangu walimchukia, kuna kipindi niligoma kabisa kuhudumia familia, akafanya mpango, akanishataki mpaka akawa anachukua nusu ya msharaa wangu.
Aliniambia pesa yake irafanya maendeleo na mimi ya kwangu itahudumia familia. Alifyeka kiwanja tukaanza kujenga, ilifikia hatua niukija na pesa nyumbani anaziiba na kwenda kuweka kwenye ujenzi, basi nilikua nagombana naye, wakati mwingine nampiga lakini alinilazimishia mpaka nyumba ikakamilika, nyumba kubwa tu tena nzuri. Lakini kabla ya kuhamia siku moja alinipigia simu.
Nakumbuka nilikua nyumbani kwa Dada yangu, sikua na kitu cha kufanya lakini kwakua kila siku nilikua nagombana na mke wangu, nilichokua nikifanya nikitoka kazini naenda kula kwa dada yangu amabye ameolewa narudi nyumbani kulala tu. Hata pesa ya matumizi nilikua nampa dada yangu na walikua wananipokea kwa furaha huku yeye nashemeji wakiniambia mabaya ya mke wangu na kumuona kama shetani.
Wakati tunakula chakula cha usiku kwa Dada mke wangu alipiga simu, alitaka kuongea na mimi lakini nilimkatia na kumuambia asinisumbue. Basi baada ya kama dakika kumi hivia linitumia meseji, “Mume wangu siko vizuri njoo tu unione hata kama hutanipeleka hospitalini!” mimi nilichukulai kama utani, nikawasomea meseji Dada na shemeji wakaanza kucheka, basi tukaongea na kucheka, nakumbuka ilikua ni kama saa nne za usiku hivi.
Basi Dada na shemeji walinipigisha stori mpaka kwenye saa saba hivi ndipo nilirudi nyumbani. Nilifika na kuanza kugonga mpango lakini haukufunguliwa. Niligonga sana lakini malngo haukufunguliwa, nilipata hasira na kuanza kutukana pale ndani, mimi nafanya kazi, na mke wangu naye alikua anafanya kazi. Nikiwa na watoto wawili, mmoja wa miaka mieili na mwingine wa miezi sita niligoma kabisa kutafuta mfanyakazi.
Mke wangua liniambia anataka mfanyakazi wa kumsaidia lakini nilimuambia kuwa, mimi sikuoa ili kuishi na wanawake wawili ndani, nilimuambia kuwa sitaki mambo ya mfanyakazi, kama akija basi namgeuza mke siwezi kula chakula cha mfanyakazi. Nilimuambia kama anachoka kufanya kazi na kuhudumia familia basi aache kazi, mke wangu mimi alikua ni Daktari hivyo mchana kutwa nakua bize lakini akirudi nataka anihudumie kama mume.
Nilikua nakula kwa Dada, nikirudi nyumbani nikakuta chakula sili nasem animeshiba, ila nikarudi kachelewa kupika au hajapika basi nitaongea mpaka asubuhi na wakati mwingine nilikua namuamsha saa tisa usikua nipikie wali, nilikau namuamrisha kuwasha mkaa kwani mimi sili chakula cha Gesi, absia likua anafanya au kipigo, hivyo alilazimika kufanya kwani mara nyingi nilikua namtishia kumuacha.
Sasa pamoja na kuwa na watoto wawili tena wadogo ambao nilimzalisha harakaharaka tena wote kwa oparesheni lakini bado nilihisi sijamkomesha, niliona kama ana chiki na mimi. Nikataka asiwe na mfanyakazi ilia ache kazi na kuwa Mama wa nyumbani. Lakini mke wangu hakuacha kazi, alilazimishia kuifanya hata kwa shida, alichokua akifanya ni asubuhia maamka saa kumi, anawapeleka watoto kwa Mama yake ambapo anapanda daladala mbili.
Akitoka hapo anapanda nyingine kwaajili ya kwenda kazini, ksiaha akitoka kazini anawapitia, nilikua na gari lakini kwakua niliamini namkomoa na nilitaka aache kazi sikutaka apande gari yangu ingawa ofisi zetu zilikua njia moja. Basi niligonga sana, alipaswa kunifungulia yeye mlango kwani, hatukua na binti wa kazi, basi niligonga sana lakini mlango haukufunguliwa. Tulikua tunaishi nyumba nzima ingawa ilikua ni ya kupanga.
Niliondoka kwa hasira kwenda kulala kwa Dada, nilifika na kuwaambia kila kitu, waliniruhusu kulala mpaka ausbuhi. Asubuhi ilikua ni lazima kurudi nyumbani kubadilisha nguo, ile kufika nakuta bado kumefungwa, nikaagonga sana lakini hakukua kumefunguliwa, mara nikamsikia mtoto wangu mkubwa wa miaka miwili analia, alikau analia ananyamaza, analia ananyamaza, nilishtuka na kuhisi kuna kitu.
Niliita majirani, wakanisaidia kuvunja mlango, kuingia ndani tu sebuleni namkuta mke wangu kalala chini. Pembeni yake alikua kampakata mtoto wangu mchanga ambaye bado alikua kashikilia titi la Mama yake nayeye kalala. Nilijaribu kumuamsha mke wangu lakini alikua ameshafariki dunia, kumuangalia mtoto bado alikau anapumua lakini kachoka. Kusema kweli nilishindwa kuvumilia presha ilipenda nikapoteza na fahamu.
Kuzinduka ndipo niliambiwa ni kweli mke wangu kafariki lakini watoto wapo salama, kumbe usiku wakati narudi walishalia mpaka kukaukia. Baada ya mazishi nilishangaa ndugu wa mke wangu wananichangamkia, walikua hawajui chochote kuhusu mimi na mke wangu, vipigo, manyanyaso na kila kitu marehemu alibaki na vitu kichwani kwake. Kusema kweli nilichanganyikwia kipindi hicho, kila nikifikiria meseji ya mke wangu nilichanganyikiwa.
Lakini sikua na namna, baada ya mazishi ilikua ni lazima maisha kuendelea. Ilibidi mazishi kufanyika kwenye nyumba yetu mpya, ilikua ni nyumba kubwa, ambayo mke wangua lichukua mkopo kazini kuimalizia, alikua kanunua karibu kila kitu kipya cha ndani, mimi nilikua najua tunajenga wakati mwingine natoa hela wkani alikua ananibana lakini sikujua kama itakua nzuri namna hiyo. Miezi minne kabla ya kumalizika nilikua sijakanyaga, ilikau ni nzuri na mipango ilikua mwezi huohuo baada ya kodi yetu kuisha tuhamie, lakini mke wangu hakuingia katike ile nyumba akiwa hai ailiingia akiwa maiti.
Niliumia sana kwani ni kama mke wangu alinijengea, lakini maisha yaliendelea, ndugu wa mke wangu walitaka kunisaidia kulea wanangu lakini ndugu zangu walikataa, niliwachukua mpaka kwa dada yangu wakawa wanaishi huko mimi natuma matumizi. Lakini huwezi amini, siku ya 40 ya mke wangu ndiyo likaja suala la vyeyti feki, nilitumia cheti cha mtu kidoato cha nne sikujua kama nayeye alikitumia basi nikafukuzwa kaqzi, sina akiba, sina mafao sina chochote.
Hapo ndipo nilijua thamani yangu, kuna kipindi nilishindwa hata kutoa matumizi ya chakula, mara Shemeji akaanza kulalamika kuwa watoto wanamchukulia muda na Dada, likaja suala la kwamba maisha magumu hana pesa, miezi sita tu nilirudishiwa watoto wangu. Nilikua sina kitu, hata kununua maziwa ya mtoto ilikua shida, sijui wapi pakuanzia maana nilifukuzwa kazi hata mafao sikupata.
Ilibidi ndugu wa mke wangu kuwachukua watoto, nililazimika kuanza Biashara, sikua na mtaji, nilichokifanya ni kutafuta mpangaji wa nyumba ambayo nilijenga na mke wangu. Kwakua ilikua nzuri nikapata mtu akawa ananilipa laki tano kwa mwezi, haikua bei yake lakini nilikua nashida, nilichukua kodi ya mwaka na hiyo ndiyo nilianza kama mtaji, nikafungua duka la vifaa vya simu kwani kuna rafiki yangu alikua akiifanya hiyo Biashara, yeye alikua akiuza simu, nikaanza na vitu vichache basi akawa ananiletea na simu dukani kwangu nazungusha mpaka leo.
Nimefanikiwa duka limekua kubwa linajiendesha maisha yameendelea. Lakini mpaka leo namkumbuka mke wangu, kwani bila yueye nisingekua na nyumba, bila yeye nisingepata mtaji kwani kodi ya nyumba aliyojenga na mimi kuchangia kwa shida ndiyo imenipa hii Biashara. Kila mtu alinikimbia na wengine niliokua nikiwasaidia walinicheka, nashukuru Mungu alinipa malaika, mke wangu ni kama alijua na kuniandalia maisha mazuri, pumzika kwa amani mke wangu, sikua mume kwako, natamani uone jinsi ninavyojutia kwa niliyokufanyia.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA