NAOMBENI USHAURI

Photo by IDDI MAKENGO🇹🇿 on September 14, 2020. Image may contain: one or more people and people standing.

naomba ushauri kama inawezekana, mimi ni kijana nina miaka 27, nilikua na mahusiano na mwanamke mmoja nilikua naishi kwake, yeye kanizidi umri kidogo ana miaka 45, nimeishi naye tangu nina miaka 20 mpaka sasa kipindi namaliza kidato cha sita akanisomesha mpaka chuo. Katika kipindi chote hicho sikujua kama ameolewa kwani mume wake walikua hawaishi pamoja, sisi tulikua tuko mwanza na mume wake alikua Kigoma.

Mara kwa mara alikua anasafiri akinidanganya kuwa anaenda kuwaona watoto wake lakini kumbe huko nako kuna mume wake. Lakini kuna kipindi watoto wake wakija alikua akiniambia kuwa nisilale naye chumba kimoja niwe na lala na mlinzi kwani hakutaka kuwachanganya kwani ni wadogo. Katika kipindi chote hicho tulibahatika kupata mtoto mmoja na mimi nilikua namsaidia kusimamia Biashara zake nikijua kuwa nikimaliza chuo na mimi kuwa na kazi yangu basi naweza kumuoa.

Baada ya kumaliza chuo nimehangaika kutafuta kazi nimekosa, ila bado nilikua na nia ya kumuoa. Nilimuomba anipeleke kwao akawa anachengachenga sana, nikaamua mwenyewe kufuatilia mpaka kwao kwa wazazi wake. Nilienda na kujitambulisha ndipo kila mtu alinishangaa kwani yeye ni mke wa mtu. Niliumia sana na kuamua kwenda kumuona mume wake cha ajabu hata mume wake hakujali akaniambia tu pole kwani yeye alishatengana na mke wake muda mrefu na walikua wanalea watoto tu kwakua mke wake ni muathirika na yeye hajaathirika.

Kaka nilichanganyikiwa na kweli nilipopima nikakutwa nimeathrika. Mimi niliikubali hali yangu na kurudi kwa mwenzangu nikamuambia kuwa nimemsamehe kwa kuniambukiza UKIMWI makusudi. Sasa tatizo na sababu ya kuja kwako nikuwa niliporudi kanifukuza eti kwnaini nimeenda kwa ndugu zake kumdhalilisha hivyo hanitaki, kanifukuza na begi tu. Nimerudi nyumbani ndugu hawanitaki, wale wote niliokua nikiwasaidia hawanitaki, hapa nimchanganyikiwa nawaza haki zangu kwa huyo dada, je si nina haki kwa kuishi naye muda wote huo, mimi bado nampenda lakini yeye hataki kunisiki atena nfanye nini kaka?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA