MWANAMKE KAMA ULIKUWA HUJUI, UPENDO WA MWANAUME NI SIKU 100.

 



Mwanamke usichokijua,mwanaume anatawaliwa na tamaa then anapenda.
Na akipenda anaga mambo mengi,yaani mwanaume akimkubali mwanamke anampitisha kwenye mchakato kwa serikali yake ya ubongo,nafsi na moyo pasipo msaada wa ndugu,jamaa au rafiki atakachokifanya ni kuwapa taarifa tu.

Mwanaume kumpenda mwanamke ni zaidi ya siku 100,siku mia ni kwa sababu sio tamaa tena ni upendo wa ndani kabisa,
Siku 100 ameshakuchambua sana,amekutathmini na amekuelewa zaidi ya wote aliowatamani.
Tabia ya kutamani kuna muda wake,tamaa ikiisha anapuuza ile speed ya kufuatilia na mbwembwe za hapa pale zinaisha.
Wanaume tunaanzaga kwa speed then speed inashuka.
So speed kushuka kiasi cha kupoa kabisa ni wazi hana jipya tena.
Hana jipya ni wazi kuna kitu alikitamani kwa haraka apate na atokomee.
Hawezi kumaliza hata siku 60 kukaa kungoja anapotea,ndio maana mwenye mapenzi anavumilia muda mrefu.

Wanawake hapa akili kumkichwa,kuna wanaume wataka tendo na wataka pendo.
Siku 100 zitatenganisha nani mtaka tendo na mtaka pendo.
Mtaka pendo ndiye mpendaji sio wa tamaa.
Pimeni kwa siku 100,msiruhusu kutumiwa kwa haraka,labda na wenyewe utake tendo tu sio pendo maana kuna mahusiano yanazaliwa sio ya kudumu ni ya kuenjoy tu faragha na kupotea.
Kama ni hivyo ni nyie wenyewe,siwapangii.
@maisha_halisitz

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA