Si kila anayeonesha kukupenda sasa anafaa kuwa mumeo au mkeo.




Si kila anayeonesha kukupenda sasa anafaa kuwa mumeo au mkeo. Elewa kwamba kuna wanawake wengine ambao wao kupenda kwao hawamaanishi ni ili waolewe, wanapenda tu na kufurahia kampani lakini ukiwatajia ndoa, usije ukashangaa wakakataa kuolewa. Hawa wa sampuli hii ukiwalizimisha utakiona cha mtemakuni.


Namaanisha kwamba, wapo wanawake ambao lile neno ndoa tu kwao limewakalia kushoto lakini wanajua kupenda na kuwaridhisha wanaume. Ni sawa na kulazimisha kumuoa changudoa ambaye ni mtaalamu wa kudatisha, mtaalamu wa kubembeleza na mtaalamu wa kumpa furaha mwanaume yeyote kwa kuwa ameona pesa. Ukimuoa mwanamke wa aina hiyo ukidhani utapata mambo kama hayohayo, umeumia.

Hilo lipo pia kwa wanaume, kuna wale ambao wanaweza kuonesha upendo wa hali ya juu lakini hawako tayari kuingia kwenye ndoa. Ukilazimisha kuolewa na mwanaume huyo, umeula wa chuya kwani huwezi kuyapata mapenzi aliyokuwa akikupa kabla ya ndoa.

Kwa maana hiyo nihitimishe kwa kusema kuwa, lazimisha ndoa lakini kwa mtu ambaye una uhakika anahitaji kuingia kwenye ndoa na umemsoma vizuri na kubaini hawezi kuja kukuletea maumivu siku za baadae.
Lakini sasa kama huitaki ndoa, hakikisha unaweka mazingira mazuri ili siku ukiwa mzee usiende kufugwa kwa ndugu kisa tu huzaa au ulizaa ila watoto hawakupata malezi ya kuja kua msaada uzeeni, omba omba wengi wa leo, wengi chanzo ni hiki hawakutegeneza familia bora za kuja kuwahifadhi uzeeni, unakuta wazaa kila mtoto na baba yake au mama yake na watoto walipokua wakawa haipendi tabia ya baba au mama yao ya kua na wanaume au wanawake wengine wakawa dharau na kuwapotezea leo uzeeni hawana msaada hivyo ndoa inafaida pia siyo ya kupuuza kama huitaki basi zingatia maneno yangu utanikumbuka
#MadamKasema
@maisha_halisitz

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA