KAMA MWANAMKE ANAKUTAFUTA KILA WAKATI AKIWA NA SHIDA FLANI BASI JUA WEWE SI MPENZI WAKE NI SPONSOR!




Kama mwanamke anakutafuta kila anapokua na shida, kila anapotaka kukuomba kitu, iwe ni kukuomba fedha au kuomba umsaidie kitu falani labda kazi au ana tatizo flani ndiyo anakutafuta. Kila ukimhitaji anakua bize, anatafuta sababu ya kutokutaka kuongea na wewe tena nzuri na ya kuaminika, lakini anapokuhitaji hizo sababu hawi nazo.

Lakini hata huo wakati mnapokua naye, kwa mfano kakuita au umemuita, kitu cha kwanza anakuambia shida yake, halafu anajifanya kuwa ana haraka, kila baada ya dakika kadhaa anaulizia kwahiyo utanisaidia lakini hata mkiwa faragha anajifanya kuwa ana mawazo na ukimuuliza anakuambia “Si nilikuambia kuwa nina shida flani”.

Kwamba hata kama umesema utamsaidia, kwa mfano akakuomba pesa na umesema utampa lakini bado najifanya kuwa shida yake inamuumiza kichwa sana kiasi cha kushindwa kuwa na wewe kiakili na hata kimwili. Ndugu yangu kama una mwanamke wa namna hii basi jua tu kuwa wewe si mpenzi wake ni mfadhili wake “Sponsor”.

Yuko nawewe kwakua anakutumia, inawezekana ana mtu mwingine ambaye anampenda lakini kwakua hamsaidii mambo yake, kwakua hamsikilizi na hamfariji kama wewe basi analazimika kukuweka wewe huku akiendelea kubembeleza kule. Utakuta muda wake mwingi anautumia kwa huyo mtu kuliko kuwa na wewe.

Lakini inawezekana hana mtu mwingine, ila hiyo haimaanishi kuwa wewe ni mtu wake hapana. Ameamua kuliko kuwa mpweke ni bora kuwa na wewe wakati akitafuta mtu mwingine wa kudumu naye. Haenjoy kuwa karibu na wewe lakini anafurahia misaada yako hivyo anaona kuwa kama akikuacha ataikosa na anaamua kukuvumilia tu.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA