NINI CHA KUFANYA PALE UNAPOGUNDUA KUWA MKE WAKO AMETEKWA KIMAPENZI NA MWANAUME MWINGINE!



Najua mnaweza kunishangaa na kuhisi labda jibu ni rahisi, ukasema mimi mke wangu akinisaliti si namuacha tu! Lakini si rahisi kiasi hicho na si kila mwanaume ana huo ujasiri wa kumuacha mke wake. Kuna wanaume wengi sana wanasalitiwa na wake zao na wameshahangaika mpaka wamechoka, wamejaribu kusuluhisha lakini wapi? Wameenda kwa ndugu wa mke na hata kuongea na michepuko ya wake zao lakini wapi!
Ndiyo kama ambavyo wanawake wengi huteseka katika ndoa zao basi kuna wanaume wengi nao huteseka. Kwa bahati mbaya wanaume huumia zaidi kwani huona aibu kutafuta msaada, huona aibu kuomba ushauri na hivyo kuvumilia. Ni ujasiri sana kwa mwanaume kukiri na kusema mke wangu ananisaliti wakati huo huo bado anaishi na huyo mwanamke. Ni aibu kwani jamii itakushangaa kukuona kama si mwanaume kamili.
Kwasababu hiyo wanaume wengi huvumilia na maumivu yao, hujaribu kuficha kwani hawana hata nguvu za kumfukuza mke. Unaweza kudhani kuwa ni wale wanaume tu ambao wanalelewa lakini hapana, wapo wengi na kazi zao nzuri lakini hawawezi kuwadhibiti wake zao. Wananyanyasika na kuteseka, mke hawezi hata kumpikia chakula au kumfulia anamdharau anachepuka wazi wazi na mwanaume hasemi chochote, kama uko katika hali hii basi hiki ndiyo chakufanya;
(1) Tafuta Sababu Ya Mke Wako Kuchepuka Hivyo; Kabla ya kufanya chochote hembu angalia ni sababu gani mke wako anachepuka, uchepukaji wa wanawake mara nyingi ni tofauti na wa wanaume, wanawake wengi huchepuka kwa sababu flani tofauti na wanaume wengi ambao ni umalaya tu. Hivyo hembu angalia kwani sababu nyingi za kuchepuka kwake inaweza kuwa ni wewe mwanaume. Sababu kubwa za wanawake kuchepuka ni kutokufikishwa kileleni, mwanamke ambaye alishawahi kufika kileleni kama usipomfikisha atachepuka tu.
Hivyo hembu angalia shughuli yako kitandani je unamfikisha? Sababu ya pili ni pesa, hapa sizungumzii mamilioni hapana nazungumzia kama je unamtimizia mahitaji yake yote ya muhimu. Lakini je yale ambayo humtimizii ni namna gani unaongea naye pale unapomuambia huna? Jambo jingine ni kujali, kama hujali hisia zake, humuoni kama mtu, unamuongelesha kama takataka, unataka kusikilizwa wewe tu, una wivu uliopitiliza kila siku wewe ni gubu tu basi huyo mwanamke atachepuka.
Angalia sababu kuona kama wewe ndiyo unasababisha au ni umalaya wake tu, usikurupuke kuongea naye kabla ya kujua tatizo ni nini? Kama ukijua sababu ya yeye kuchepuka, ukajua kuwa ni wewe basi kitu cha kwanza kabla ya kuongea naye hembu amua kubadilika, angalia yale mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wako badilika na yafanye. Kuna ambayo yako nnje ya uwezo wako na huwezi kumtimizia basi ongea naye kuhusu hayo.
(2) Mkalishe Chini Na Ongea Naye; Umeshafanya uchunguzi, umejua na sababu au hukujua lakini unaona kuwa bado ana mtu yuko naye, labda ni mmoja au wawili. Hatua ya pili ni kuongea naye, muambie kuwa unajua kua anachepuka, lakini kama nayeye anajua kuwa unajua muambie kuwa umeshachoka na tabia yake hivyo unataka muongee, unataka akuambie tatizo hasa ni nini? Hata kama ulishajua tatizo lakini hembu mpe nafasi aongee, umsikie nayeye.
Hapa jaribu kushusha hasira, ongea kama unataka suluhu na si kama vile unataka kumpiga au kumuacha. Najua ni ngumu. Labda ulishaongea naye kabla, labda hata ulishampiga lakini hakujali. Sasa ongea naye na muambie unataka aseme yeye anataka nini hasa, akuambie kama amechoka ndoa au la. Kama akikuambia amechoka ndoa na anataka muachane basi usipaniki, muambie ni namna gani anataka muachane, kama mna watoto muongee itakuaje, kua mtulivu kila wakati hata kama atataka kukukera.
(3) Mpe Msimamo Wako; Baada ya kuongea, mnaweza kufikia muafaka au hata msifikie, vyovyote itakavyokua wewe kama mwanaume nilazima utoe maamuzi yako ya mwisho. Umuambie kabisa kuwa wewe umeamua nini, kama kuna mambo amekuambia kuwa unapaswa kubadilika na unaona kama yanawezekana basi muahidi utabadilika. Lakini muambie kuwa yale ndiyo nyatakua mazungumzo yako ya mwisho kuhusu hilo swala, kwamba yeye aachane na huyo mtu au asiachane naye hutalizungumzia tena hilo suala na unaamini kua amekuelewa, muambie msimamo wako, mamauzi ambayo utayachukua kama hatabadilika.
(4) Mpe Muda Wa Kubadilika Usimfuatilie Akajua; Baada ya kuongea naye anategemea kwamba utaanza kumfuatikia, kushika simu zake na kumkataza baadhi ya mambo, inawezekana hata wewe ungetaka kufanya hivyo, hapana huo si uamuzi sahihi. Ni kitu ambacho anakitegemea hivyo atakua makini zaidi, lakini ni kitu ambacho anakitaka. Kisaikolojia unapomfuatilia mtu anajua kuwa bado unampenda na unamhangaikia.
Unatakiwa kurudi nyuma kidogo, mwanamke na hata mwanaume anatakiwa kufahamu kuwa huogopi kumpoteza. Kwamba hata kama unampenda vipi, hata kama inakuumiza vipi lakini hujali sana, una maisha mengine ambayo hata hayamhusu. Sasa ukishaongea naye na kumpa msimamo wako, unapaswa sasa kurudi hatua moja nyuma. Kama ulikua unashika simu yake acha, kama ulikua unamkataza kutoka, kufanya kazi na vitu kama hivyo acha.
Najua unashangaa lakini fanya vitu kinyume na ambavyo angetarajia. Katika kipindi hiki mpe muda, kwamba uanweza kusema nampa miezi mitatu kama hatabadilika basi natekeleza maamuzi ambayo ulishamuambia. Humuambii kua na kupa muda gani hapana huu ni muda ambao unajiambia wewe. Katika muda huu pamoja na kwamba humfuatilii wazi wazi lakini mfuatilie kimyakimya, angalia kama kabadilika au la.
Hakikisha anajua kuwa hujali humfuatilii, umemkatia na umechoka kumbe chini chini unamfuatilia na kutaka kujua kila kitu. Hii itamfanya ajifikirie mara mbili kwani wakati mwingine anakunyanyasa na kukuumiza, anafanya mambo ya kukukera kwakua anadhani kua kashakuweka mkononi kakukalia na inawezekana hata kuna Kadawa alishapewa hivyo anajua huchomoki. Ukiacha kumfuatilia waziwazi na kunyesha huogopi kumpoteza kama bado anakupenda atabadililika na kama hakupendi hatajali ataendelea na mambo yake.
(5) Mpeleke Kwa Mchepuko Wake/Mrudishe Kwao; Kwa wanaume wengi wakimchoka mwanamke anamrudisha kwao, hili linaweza kuwa ni wazo zuri lakini anaweza asijifunze, unatakiwa kumfudnisha kitu kuhusu mchepuko wake. Kama anayo mingi chagua mmoja, umechunguza umejua kuwa mke wako anatembea na flani. Usiku mmoja baada ya ule muda wako uliojipa kupita na umeona kuwa habadiliki basi mpeleke huko.
Kama una Gari mpakie na kama huna tafuta usafiri, muombe akusindikize sehemu kisha ondoka naye mpaka kwenye nyumba ya yule mtu. Ukifika gonga na mlango ukifunguliwa bila kujali kama yuko na mkewe au la muambie kuwa nimekuletea mtu wako, mimi kashanishinda hivyo nimekuletea ili uwe huru naye. Mwanamke hapa anatakiwa kujua kuwa wewe nawe ni kama shetani hivi, hivyo hakikisha unaonyesha huna sura ya huruma.
Uksihamkabidhi muache hapo na ondoka, kama una ujasiri wa kufanya hivi jua kuwa atafukuzwa pale kwani hata kama jamaa hajaoa hatataka mwanamke ambaye kakataliwa na mwanaume mwingine. Kama na mke ni moja kwa moja hatataka hata aingie ndani kwani atamharibia ndoa yake lakini kama hajaoa basi ataona kama ni kaletewa mzigo hivyo atajaribu kuukwepa kwani nina uhakika ana mpenzi wake na hapo mkeo ndiyo ataona kuwa kumbe yeye si Keki kama alivyokua anadhani.
Lakini kama hujui ilipo michepuko yake basi mrudishe kwao kama ni karibu na muambie kuwa umechoka, wakabidhi mtoto wao basi. Kama kwao ni Kijijini basi tafuta sababu ya kwenda, kusanya nauli yako na kisha muombe hata muende kusalimia, unataka kuongea na wazazi wake na mambo kama hayo. Mpeleke na ukifika hata usitake mazungumzo mkabidhi na ondoka zako. Usitake mazungumzo na waambie kuwa umechoka na hutaki tena suluhisho.
(6) Kama Anakupenda Atabadilika Kama Hakupendi Hatarudi; Najua kama unampenda mtu sana utaogopa, labda nikimpeleka ndiyo nitampa uhuru wa kufanya mapenzi na michepuko yake, labda hatarudi, vipi kuhusu watoto na mambo mengine mengi. Lakini kama ambavyo huwa nawaambia wanawake kuwa mtu akishakuchoka kakuchoka, ni maamuzi yako kuendelea kuishi kwa mateso na maumivu mpaka pale atakapokueletea UKIMWI na kaumua kubadilika au pale atakapokuacha wewe au kumuacha uumie utapona baadaye.
Kama umefanya yote hayo naamini kama mwanamke anakupenda atarudi na kukuomba msamaha, lakini kama ummefanya yote haya na hajarudi basi mshukuru Mungu kwani huyo mwanamke hakua ni fungu lako. Hata kama ungeendelea kukaa naye basi usingekua na furaha katika maisha yako. Nilazima wakati mwingine ujifunze kuseama kuwa inatosha hata kama inauma sana, nilazima ukubaliane na hali kuwa si kila mtu ambaye unampenda atakupenda hivyo hivyo na ni sawa kumuacha mtu aende.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA