KABLA YA KUJIULIZA NI KWANINI ANAKUSALITI MARA KWA MARA HEMBU JIULIZE KWANZA NI KWANINI UNAMSAMEHE MARA KWA MARA?



Hili ni swalia mbalo naulizwa kila siku, ukiingia katika inbox yangu utakuta asilimia tisini ya meseji ni za wanawake ambao huniuliza kuhusu kusalitiwa. Mwingine atakuambia kuwa nimemfumania mume wangu na Dada wa kazi, mwingine mume wangu bado anawasiliana na X wake mpaka anafikia kunipigia simu na kunitukana. Mwingine mumewe anatembea na vitoto vya shule na hataki kuacha, mwingine mumewe kawekwa kinyumba na mwanamke huko!
Mwingine ni mchumba wake anamsaliti, kila sikua nakuta meseji za wanawake wengine, mwingine ni jirani yake anatembea na mumewe. Mwingine mchumba wake kazaa na mwanamke mwingine lakini bado anamuambia anampenda. Maswali ni mengi kuhusu usaliti na mara nyingi wanawake wanaoomba ushauri wanakua bado wapo katika ndoa au hayo mahusiano ya kusalitiwa, wanawasamehe wanaume kila siku.
Kwangu kumsamehe mtu si shida, lakini Dada zangu, kwa wale niliowajibu na hata ambao bado meseji zenu sijawajibu nataka mnijibu au mjiulize swali moja. “Kwanini unamsamehe huyo mwanaume?” Hili ni swali la muhimu sana kwani litakufanya ujielewe wewe kama mwanamke. Hembu kwa wale ambao mshasalitiwa hata kama hamtasema hapa lakini jiambie au tafuta jibu ni kwanini ulimsamehe mwenza wako mara ya kwanza?
Lakini kwa wale ambao hamjawahi kusalitiwa au ambao hamjui kama mnasalitiwa, mjiulize je ukimfumania mume au mpenzi wako utamsamehe? Kama jibu ni ndiyo jiulize kwanini na kama jibu ni hapana basi jiulize kwanini? Wengi najua mtaseama akiniomba msamaha nitamsamehe au aliniomba msamaha na kuniambia hatarudia tena. Lakini tuongee ukweli je hiyo ndiyo sababu halisi kweli ya kumsamehe? Alikuambia hatarudia akarudia lakini bado ukamsamehe kwanini?
Hakuna kitu kingine kweli kimekufanya umsamehe? Nakuuliza kwakua hicho kitu kingine ndiyo ambacho kinamfanya huyo mwanaume kukunyanyasa kila siku, kama hutajua kwanini kila akikusaliti unamsamehe basi jua wewe utakua ni mtu wa kulia tu. Labda twende taratibu ili mnielewe Dada zangu, maswali ni mengi na siwezi jibu mmoja mmoja lakini hembu tuponyane mazima hapa, umemsamehe kwanini?
Umesema ni kwasababu ameomba msamaha, hapana mimi sidhani kama ni sababu. Lakini kuna hii sababu nyingine, mnasema “Wanaume wote wako hivyo utaacha wangapi?” Hata hisa ikubaliani nayo, labda nikupe sababu ya kwanza, hembu iangalie kama kwako ni sababu. Mimi nadhani nikwakua unamtegemea huyo mwanaume kikipato, hapa sisemi hufanyi kazi hapana? Kazi unafanya napengine una mshahara mkubwa zaidi yake.
Lakini pamoja na kipato chako au huna kipato unamtegemea kukufanyia maamuzi yote, kila kitu kinapitia kwake mpaka unawaza hivi nikimuacha nitaweza kuishi mwenyewe kweli? Hii ndiyo sababu kubwa kwa wengi, kuogopa kuondoka kwakua wanaogopa maisha. Hembu jiulize je hii ndiyo sababu yako? Kama ndiyo hii basi kama hutakua huru kikipato huyo mwanaume hataacha kuchepuka kwani kila wakati anajua kua huwezi ondoka.
Utaenda wapi wakati aina ya maisha unayoishi unamtegemea yeye. Sababu ya pili halisi ninayoiona kwa wengi ni kuogopa macho ya watu, unaona kama ukiachika utaonekana kama umeshindwa, kwamba hufai, unaogopa kuambiwa kuwa aliolewa akaachika. Sababu nyingine nikuogopa maisha ya peke yako, kila wakati unaona kuwa kama ukiachika ni ngumu sana kupata mwanaume mwingine, unawaza namna ulivyompata huyo kwa shida unaona hapana!
Unaona kama nikiondoka nitakua peke yangu milele, una uoga. Kuna kundi jingine ambalo ni la kuwaza watoto, hii mimi naona si sababu halisi na mara nyingi ni kisingizio kwa wanawake ambao huogopa kuishi peke yao, inarudi kule kule kwenye kipato. Najua huamini lakini ukiwaza kuwa labda ukiondoka na watoto hatawahudumia au hata ukiondoka akiwang’ang’ania huwezi kuwapigania kwakua huna kipato kama yeye.
Mwisho ninachotaka kusema hapa nikuwa kama mume wako kakusaliti kabla sijakuambia nini cha kufanya hembu anza kujiuliza ni kwanini unavumilia? Je ni kwakua unampenda sana, kwakua unaogopa kuishi peke yako, kwakua huna kazi na unamtegemea yeye, kwakua unaogopa macho ya watu au chochote kile. Nataka ujiulize kwakua jibu utakalolipata hapo ndiyo ambalo litakusaidia kupambana na kuchepuka kwake.
Mimi kukuambia kuwa ondoka muache hakuwezi kusaidia kama ukiondoka hapo huna hata hela ya kupanga, mimi nikikuambia kuwa pambana uchukue wanao haitakua na maana kama ukiwachukua huna pa kuwapeleka zaidi ya kwenda kuwatupa kwa Mama yako na kuwa mzigo tena. Sijui mnanielewa, hembu jiulize je nikwanini nimsamehe huyu mwanaume, tafuta sababu na ukiipata basi nirahisi kuibadilisha na hatakunyanyasa tena.
Sababu wewe kumsamehe ndiyo udhaifu wako, sasa kama hujui udhaifu wako ni upi basi ni ngumu huyo mwanaume kukuheshimu kwani anajua kuwa hata nikimsaliti mwisho wa siku udhaifu wake ni kitu flani nitautumia na kumuomba msamaha au hata sitaomba msamaha lakini atanisameje. Sisemi uanze kuwaza kumuacha mume wako hapana ninachosema ni uanze kuwaza ni kwanini unamsamehe kabla ya kuwaza kwanini anakusaliti!
13

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA