SUALA LA TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO

💞 *MASUALA YA NDOA*💞
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
*JIMAI WAKATI MWANAMKE ANA MIMBA*



Hakuna tatizo kabisa kishari’ah kwa mume kumuingilia mkewe wakati ana mimba hata ikiwa atazaa kesho. Itakatazwa tu ikiwa labda mke ana matatizo na kujimai wakati huo ima kwa kuumia au kudhurika.
Ama kuhusiana na wakati wa jimai, Uislamu haukuweka wakati maalumu ila hayo yanategemea masikizano yenu nyinyi wanandoa. Mnaweza kufanya baada ya Alfajiri au kabla yake, baada ya Dhuhr au baada ya ‘Ishaa au wakati mwengine wowote. Kinachokatazwa ni kufanya jimai wakati wa Swalah hivyo kuikosa au wakati ambao mmefunga Funga ya faradhi.
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameagizia kuwa mke asikatae kumstarehesha mumewe hata akiwa kwenye tanuri. Hii ina maana kuwa ikiwa mume amerudi nyumbani na mke yuko jikoni, mume anapomtaka inabidi atoke huko kwenye kazi yake ili kumkidhia haja mumewe.
_*Na Allaah Anajua zaidi*_

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA