IJUE TOFAUTI YA MAPENZI NA UPENDO

Kwanza kabisa nianze kwa kusema jambo moja kuu;-


Mtu unapokuwa na shauku ya MAPENZI ni eneo linalotokana na tamaa ya mwili pamoja na hisia juu ya hitaji husika la NGONO

Na mtu aliyewaka tamaa ya NGONO hawezi kuzalisha UPENDO WA MOYONI ila anaweza kuzalisha UPENDO WA MWILI maana hata mapenzi bila kuyapenda nadhani huwezi kuwa na sababu ya kuwa na mtu

Lakini pia UPENDO ni zao la haja ya moyo na mara zote huwa naamini MWENYE UPENDO NI RAHISI KUTOA PENZI LENYE MAANA ZAIDI kwa sababu kilichozaliwa ndani yake ni UTASHI na kama mwenye UPENDO akiwa katika kweli yake swala linaitwa MAPENZI hutokana na utimilifu wa adhima yake ikiwemo kusubiri.
Kuna watu wanayataka MAPENZI kwa kisingizio cha UPENDO ila wenye UPENDO WA DHATI hawaangaliii katika MAPENZI maana ni rahisi MAPENZI kutengenezwa katika UPENDO

Ila ni ngumu sana MAPENZI KUTENGENEZA UPENDO NJE YA NGONO na hapo ndipo anguko la maana halisi ya UPENDO HUANZIAA.
Mwili unapowaka tamaa ya NGONO akili huyumbishwa kiasi kwamba Mtu unaweza kuamini UNAMPENDA Mtu fulani na kumbe akikupatia hitaji lako AUTOMATICALLY ile hali ulikuwa unaisikia inatoweka



Na JOTO LA UPENDO
likipanda juu ya mtu fulani shauku yako ni kutaka kujua kama UPO KWENYE MOYO WAKE PIA na mara nyingi mwenye UPENDO WA DHATI
akiisha pewa nafasi huongelea hatma ya safari ya MAISHA wala sio NGONO maana anaamini mwisho wa siku ni UMILIKI WA KUDUMU



Ndo maana hata Maandiko Matakatifu yanasema :-
