NJIA 5 ZA KUFAHAMU KAMA MCHUMBA ULIYENAYE ANAKUPENDA KWELI KUPITIA MANENO YAKE



Moja kati ya vitu vigumu kwa mwanadamu ni kufahamu anachokiwaza mwenzio, ingawa baadhi ya watu ni wasaanii sana kwenye uhusiano hasa wakati wa uchumba na ni vigumu wakati mwingine kutofautisha kati ya ukweli na uongo, njia hizi ni kati ya njia unazoweza kutumia kumpima kwa tahadhari mchumba ambaye unategemea awe mkeo/mmeo.
1. ANGALIA KAMA ANAZUNGUMZIA MARA KWA MARA MIPANGO YENU YA MAISHA YA BAADAE
Kama mchumba yuko serious na mpango wa ndoa, mara nyingi utamsikia akiongelea mipango yenu ya baadae kama mtu mme na mke. Kila atakachokua anapanga mara nyingi atakuhusisha na kutumia mifano ya pamoja zaidi. Angalia pia jinsi anavyopanga kuanzia vitu anavyotaka kununua hadi maongezi yake na watu wa karibu awakiwemo wazazi wake. Mtavyokuwa honeymoon, idadi ya watoto, kazi na mpangilio wenu wa maisha hadi uzeeni pamoja.
Hapo utagundua kweli yuko committed na wewe na anapanga muoane kweli.
2. ZIANGALIE SIFA ANAZOKUPA NA UZICHAMBUE.
Mchumba wa kweli anapokusifia hataishi kukusifia kuhusu muonekano wako na uzuri wako, au mitindo ya nywele na marashi tu. Mara nyingi utamsikia akitoa sifa pia kwa mawazo unayompa na uwezo wako wa kufikiria pale anapokuhusisha kwenye mipango yako. Yaani sifa zinavuka mipaka ya mwili wako kwa kuwa haishii kuvutiwa na mwili wako pekee, anaangalia umuhimu wako kwake hata baadae.
3. ANGALIA JINSI ANAVYOKWAMBIA ‘NAKUPENDA’-MUANGALIE MACHONI, SIO USONI UTAONA KITU
Kuna tofauti kubwa kati ya kukwambia ‘nakupenda’ na kumaanisha kuwa anakupenda. Angalisa sana ni nyakati gani anakwambia anakupenda na sababu anazokupa. Angalia kama anakwambia ‘anakupenda’ hata baada ya kutofautiana kimawazo. Kama anakwambia anakupenda wakati mnapokutana kwa ajili ya kitu fulani au anapotaka kukushawishi kufanya kitu fulani tu ‘shituka’.
Wataalamu wa saikolojia wanaeleza kuwa macho yanapogongana huongea lugha rahisi sana ingawa kuitafsiri kunahitaji uwe makini. Angalia anavyokwambia anakupenda huku ukimuangalia machoni moja kwa moja. Isome kwa umakini lugha ya macho yake…tutakueleza siku moja hapa undani wa lugha ya macho katika mapenzi.
4. ZINGATIA SANA MAONGEZI YAKE NA MAWASILIANO YENU UNAPOKUWA MBALI NAE..
Angalia kama kuna mabadiliko ya maongezi na mawasiliano pale mnapokuwa mbali kwa muda. Umbali unaweza kuwa chanzo cha kuwatenga kweli au unaweza kuwa chachu ya kukoleza mapenzi yenu kwa kuwa ni wachumba mnaotamani kuishi pamoja kama mume na mke hivi karibuni.
5. ANGALIA KAMA ANA UWEZO WA KUKWAMBIA WAZI PALE UNAPOKOSEA..
Kama mchumba wako wa kweli anataka kuishi na wewe kama mmeo/mkeo hatashindwa kukwambia wazi kwa lugha nzuri pale unapokosea. Hii ni kwa sababu anaona kabisa mabadiliko yako yana maana kubwa sana kwenye maisha yake kwa kuwa wewe na yeye mtakuwa kitu kimoja hivi karibuni. Usipende kupata mtazamo chanya tu kila wakati kutoka kwake, pokea changamoto za mtazamo wake kama sehemu nzuri ya kudumisha uhusiano wenu. Kusifiwa pekee kila wakati hata unapokosea ni sehemu ya uongo utakaokugharimu baadae.
6. ANGALIA KAMA ANATHAMINI MAONI YAKO
Mtu anaekupenda kweli hukushirikisha kwenye mipango yako kama tulivyoeleza hapo juu, lakini pia ni vyema kumpima jinsi anavyoyathamini mawazo yake. Angalia anavyoyachukulia mawazo yako kuanzia mawazo ya machaguo ya mavazi hadi mtazamo wa juu wa nchi. Kama anathamini mchango wako wa mawazo, utaona mara kadhaa akikushirikisha kwenye mipango yake kwa nia ya kukuomba ushauri au kufahamu mtazamo wako.
Hata hivyo, sio lazima akuulize mawazo yako kwenye kila kitu, atakuuliza kwenye mambo ambayo kweli yanahitaji mawazo yako.
Endelea kufuatilia ukurasa huu, tutakueleza kwa upande wa vitendo.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA