CHAKUFANYA ILI PESA ZISIKUPE TABIA MBAYA.
1.Tosheka na kiwango cha pesa unachokipata kwa wakati huo, usiwe na tamaa ya kutaka upate vingi kwa harakaharaka
*1 Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.*
WASHWAHILI WALISEMA HARAKA HARAKA HAINA BARAKA, TOSHEKA NA KILE UKIPATACHO.
Kumbuka: Utajiri huja kutokana na mipango ya mda mrefu aliyokuwanayo mtu hivyo usijaribu kulazimisha uwe tajiri haraka *utapitia shortcut ambayo mwisho wake ni mauti*
Utakuta mtu amepata ajira ya mshahara wa laki mbili na nusu ghafla anataka aendeshe magari yake au awe na majumba yake mh!? hapo mawazo ya kuiibia ofisi iliyokuajili yatakuingia tu.
*Hivyo epuka tamaa*
2.KUBALI KUJAZWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
Ukiwa na Roho mtakatifu ndani yako hautaweza kuzitimiza tamaa za mwili na badala yake utamzalia Mungu matunda mema.
*Wagalatia 5:22-23*
*22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,*
*23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.*
Matokeo ya kuwa na tunda la Roho ni kwamba Pesa haiwezi kukubadili kitabia na zaidi kadri unavyoipata ndivyo unavyozidi kuwa na wema, Ucha Mungu, unyenyekevu, Upendo kwa wengine, kuwa mtii wa sheria za Mungu n.k hivyo dawa ya tabia mbaya zitokanazo na Pesa ni wewe kujazwa nguvu za Roho mtakatifu
*1 Timotheo 6:17-18*
*17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.*
*18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;*
3.KUJENGA MAZOEA YA KUJIOMBEA USIINGIE MAJARIBUNI
*Luka 22:40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.*
Sisi ni wanadamu unaweza ukazipata Pesa ukajaribiwa na udhaifu wa mwili ukajikuta
*-Unakuwa mchoyo kuliko ulivyokuwa kabla*
"Luka 12:15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."
*-Unakula zaka ya Mungu kuliko hapo awali*
*-Unaachana na kumtumikia Mungu*
*-Unaachana na kuomba*
*-Unaachana na ibada*
*-Unawadharau watu ikiwemo na mchungaji wako*
*-Anakuwa mlevi*
*-Unakuwa na kiburi cha uzima* n.k
HIVYO ILI UEPUKE MAJARIBU HAYA YATOKANAYO NA FEDHA NI WEWE KUJENGA MAZOEA YA KUJIOMBEA USIINGIE MAJARIBUNI
Ndiyo maana mtunga mithali akaomba hivi
*Mithali 30:8-9*
*8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.*
*9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.*
Huyu mtu aliomba Mungu ampe mafanikio ya kati ambayo hayawezi kumuingiza majaribuni
KWAHIYO
Wewe usiye na mafanikio jifunze kumuomba Mungu akuepushe na tamaa ya kutafuta Pesa kwa njia zisizo sahihi na akupe mafanikio yasiyokutenga na utukufu wake
Na wewe mwenye mafanikio jifunze kumuomba Mungu akuepushe na majaribu mbalimbali yanayoweza kukutenga na utukufu wa Mungu.
MWISHO
NAKUOMBEA WEWE AMBAYE UCHUMI WAKO HAUKO SAWA SAWA MUNGU AKAFUNGUE MILANGO YA BARAKA ZAKO ILI ZIJE FURUSA MBALIMBALI ZA KUKUINGIZIA KIPATO KWA JINA LA YESU,
NA WEWE MWENYE UCHUMI MZURI MUNGU AKAKUONDOLEE KIBURI CHA UZIMA BALI AKAKUPE MOYO ULIOPONDEKA KAMA DAUDI KWA JINA LA YESU
Mungu awabariki sana