KUNA WAKATI ILI KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA NILAZIMA UAJIRI MTU AMBAYE HUMUAMINI!




Nilishakata tamaa ya kufanya biashara, mimi nafanyakazi katika mgodi hivyo mara nyingi nakua kazini na sina muda wa kutoka. Tangu mwaka 2015 nilipoajiriwa nilikua na hamu sana ya kufanya biashara, mtaji nilikua nao hivyo ili nisiibiwe nilitafuta ndugu yangu ilia nisaidie kusimamia biashara zangu, lakini cha ajabu nikuwa nilikua kama kila siku nawekeza lakini hakuna kitu, mara wamepata hasara, mara wameibiwa, mara nilipata tatizo, nilikua na Hardwear ambayo niliwekeza kwa zaidi ya milioni kumi nikafunga.

Nikaja kufungua duka la nguo nalo pia nikamuweka Dada yangu ambaye nilikua namuamini zaidi nikafunga, nikaja kufungua duka la spea za Pikipiki nalo likaisha nikataka kufunga. Kabla ya kufunga kuna mtu aliniambia niongee na wewe, nilikupigia ukaniambia ninunue Kitabu kwanza, sikua nikikihitaji lakini nilinunua baada ya kuongea nawe uliniambia kuwa si kila wakati unahitaji mtu ambaye utanamuamini katika kusimamia biashara yako.

Ukaniuliza kama nilishawahi kwenda Benki, nikakuambia ndiyo ukaniambia unaona kuwa wanafunga kamera ili kuwaangalia watumishi wao nikasema ndiyo ukaniuliza kwanini? Nikakuambia nikwakua hawawaamini hivyo wanachukua tahadhari? Ukaniliza sasa kama hawawaamini kwanini wakawaajiri na kwanini wanapata faida kila mwaka, sikua na jibu ukaniambia nikwakua wale wafanyakazi pamoja na kushika pesa nyingi lakini wanaogopa kuiba kwani hawaaminiwi.

Ukaniambia kuwa unapoajiri ndugu inamaana unamuamini, unaamini kua hatakufanyia kitu kibaya kwakua ni ndugu, lakini unasahau kua ndugu nao ni binadamu na hata hao wezi ni ndugu wa watu hivyo natakiwa kuajiri mtu ambaye sitamuamini ili nimchunge nayeye ajue kabisa haaminiwi ilia jichunge na ajue kabisa kama akiiba basi atafungwa. Kama ambavyo wafanyakazi wa Benki wanaogopa kuiba basi hata katika biashara yangu basi niweke mtu anayeogopa kuiba.

Uliniambia nitafute mtu ambaye anaweza biashara, mtu ambaye si ndugu, nitafute mwanasheria, tuandikishe mkataba, awe na wadhamini ambao wanamfahamu na hata ikiwezekana kwao na si sehemu anayoishi. Baada ya hapo niwe namlipa mshahara na kumfanyia ukaguzi kila ninapopata nafasi hata kama ni wakushtukiza, awe anaweka mahesabu na kila mara anaponunua mzigo nilazima kuwasiliana na mimi, ukaniambia nimtengenezee mfumo flani wa kiofisi flani.

Kwamba awe anaweka mahesbu ya kila siku na kila baada ya wiki moja awe ananitumia ripoti ya wiki. Tuliongea mambo mengi sana na nilikuelewa, niliamua kufanyia kazi mawazo yako, ilikua ni mwaka jana kwakua bado nilikua na mtaji niliendeleza duka la spea za bodaboda nashukuru ulinisaidia kila hatua. Mwezi uliopita mkataba wangu uliisha na sikupata mkataba mpya kwani wanapunguza watu, nimerudi niko kwenye biashara, biashara imesimama huwezi amini.

Uliniambia awe anawajibika kwangu na hata Mama yangu mzazi asiingize mguu au kuwa na amri kwake, ndugu walinichukia na kunisema lakini sasa wananielewa kwani naweza hata kuuza Pikipiki kwasasa. Katika kipindi hiki ambacho nimeajiri mtu ambaye simuamini nimepata faida mara mia kuliko nilipoajiri ndugu, zawadi yako nishakutumia na Mungu azidi kukubariki kwani sijui ningeishije bila ajira lakini kwasasa hata ajira sitamani.

NB: Si kila ndugu ni mwizi lakini kama umeajiri ndugu na unaona mambo hayaendi kila siku ni visababu sababu basi huna haja ya kukata tamaa, badala ya kufunga biashara basi njoo tuongee inawezekana tatizo ni kubwa zaidi ya hilo au unahitaji kuajiri tu mtu ambaye humuamini. Bei ya Kitabu ni elfu kumi tu kukipata Kitabu changu unalipia kwa M-Pesa No. 0742-381-155 au Tigo Pesa No. 0657-552-222 na ukishalipa Kitabu unatumiwa kwa Whatsapp, Email au Facebook.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA