NILIAMKA SHEMEJI YANGU ALIPOKUJA CHUMBANI KWANGU!



Baada ya kumaliza chuo nilikaa kwa Dada yangu kwa miaka miwili nikitafuta kazi, shemeji yangu alikua akiniambia ataniunganisha kazi kwa marafiki zake lakini miaka miwili ilipita bila kufanya hivyo. Nilikua nimekata tamaa, nilikua kwenye mahusiano na kijana ambaye tulisoma naye chuo, naye alikua hana kazi kama mimi.

Kila siku tulikua tunagombana kwani nikimuomba pesa akiniambia hana nahisi kama hanipendi kwani nilikua nikijiambia mwanaume utakosaje pesa! Kwakua sikua na mtu mwingine basi nilibaki naye ila nilikua naamini kuwa hanipendi na ana wanawake wengine. Kuna siku rafiki yangu aliniambia nikusome na ninunue Kitabu chako.

Mwanzo wakati nakusoma niliona unaandika vitu vya mapenzi na Biashara unazoshauri ni zile za watu wa chini ambao si waosmi hivyo nilikupuuzia, lakini kuna siku nikaamua kununua Kitabu chako cha Biashara. Kusema kweli sikukielewa chochote, nikakupigia simu kuongea na wewe ukanizungusha zungusha sijui nipigie linin a lini nikaona huyu tapeli tu hana jipya nikajikalia zangu.

Lakini mwaka jana mwanzoni kuna ishu ilitokea, shemeji yangu alikuja chumbani kwangu, aliingia bila kugonga, mimi nalala na mtoto wake wakike lakini aliingia nikiwa nimelala akaanza kunishikashika. Nilishtuka akakimbia ila asubuhi alinichekea kama ananitaka, akanitumia meseji kuwa atanipa mtaji ila anataka tusafiri wote.

Basi hapo ndipo nilijua namimi nimekua waleee ambao wanatembea na mashemeji, zao, nikikumbuka dada yangu alivyohangaika na mimi nikaanza kukupigia kilazima ili kuongea na wewe na kwa bahati nilikupata, nikakuambia jambo langu ukaniambia nisimuambie dada yangu kwani haitasaidia ila niondoke, nitafute namna ya kuondoka na kutafuta cha kufanya.

Niliwaza nifanye nini sikua na jibu, ila ukaniuliza mimi naweza kufanya kitu gani, nikakuambia napenda kusuka na marafiki wengi wadada mimi ndiyo nawasuka, najua kusuka kila mtindo. Ukaniambia maneno ambayo sasa hivi yananipa kula “Wewe ni saluni” kweli nilianza kusuka kwa pesa. Katika Kitabu chako kuna sehemu uansema mtu anaweza kujiajiri kupitia kipaji au ujuzi wake.

Uliniambia kuwa kila mtu ninayemsuka niwe nampiga picha natuma status naweka na bei ya kusuka. Uliniuliza kuhusu hao marafiki zake ni watu wa aina gani ili nijue namna ya kupanga bei nikakuambia ukaniambia nisisuke chini ya elfu ishirini kutegemea na mtindo. Kwanza niliogopa kwakua sina saluni na nilihisi Dada atakasirika.

Nilipomuambia kuhusu kusuka akaniambia nianze nayeye, akanilipa elfu thelathini nikamsuka, nilikua namsuka Bure ila akanilipa. Aliniambia nianze na yeye na atakua akinitangaza kwa marafiki zake kwani kama yeye anayenilisha ananilipa wao ni akina kani wasinilipe. Nilimpiga picha na kupost status na insta, yeye pia alipost na bei.

Nakumbuka uliniambia naweza kujiita Mobile saloon, kwa wafanyakazi na watu ambao wapo bize basi mimi nawafuata, kusema kweli ninashukuru Mungu kwani ninapata chakwangu. Nilijikusanya nikapata kodi nikamuambia dada yangu kuwa naondoka, ni kama alipata ahueni kidogo. Wakati naondoka nashangaa aliniomba msamaha kuhusu tabia za mume wake.

Nilishangaa kwani sikumuambia ndipo aliniambia ni kawaida yake kutongoza hata wadada wa kazi, aliona meseji alizokua ananitumia na majibu yake. Kumbe nilipomuambia kuhusu kusuka alijua natafuta namna ya kuondoka kwakua mwanae alimuambia kuwa mume wake alikuja chumbani nikamfukuza. Nilijisikia vibaya sana, niliona aibu ila nashukuru Mungu nimeondoka.

Bado nasuka, na nimekutafuta ili unielekeze namna ya kufungua Page Instagram na kupata wataja kwani sehemu ninayopata wateja wengi ni Whatsapp ila nataka kupanuka. Najikusanya ili nifungue saluni yangu ingawa mtaji bado sana lakini nishakata tamaa kuhusu kuajiriwa nimeamua kujiajiri na kipaji changu. Pia naomba unielekeze kama naweza kuchanga tukafungua saluni na rafiki yangu na tufungueje?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA