NJIA YA KWANZA KUMLINDA MWANAO NI KUONGEA NAYE NA KUWA RAFIKI YAKE!



Watoto wengi wananyanyaswa na watu wao wa karibu, watu ambao mzazi anawaamini na hajisikii vibaya kuwaachian watoto. Hii huwa ngumu sana kwa mtoto kuongea kwani anaona kuwa hataaminika hivyo akitishwa kidogo basi hukaa kimya. Ila kama mzazi unapaswa kuongea na mwanao.

(1) Usiogope kuniambia kitu chochote mwanangu, ukiwa na shida yoyote au kitu kikitokea niambie, wala sitakupiga.

(2) Mtu yoyote akikuambia maneno mabaya na kukuambia usiniambia mimi mbasi jua kuwa unatakiwa kuniambia, sitakuchapa ukiongea na mimi.

(3) Shuleni, hapa nyumbani au huko mnakoenda kucheza kama mtu akikugusa sehemu mbaya, kama mtu akikuambia mfanye kitu kibaya basi niambie, hata kama ni Mama yako au ni Baba yako (inategemea na mzazi unayeongea) niambie na wala usiogope.

Pia mzazi unaweza kutumia mbinu nyingine kwa kumuuliza mtoto maswali ya klijanja janja kama hivi.

(1) Shuleni mkifika mnafanya nini wakati wa mapumziko, rafiki zako ni akina nani, mnapocheza mnacheza michezo gani?

(2) Dada anapokuogesha anakuogeshaje, anakuogesha vizuri kweli? Hembu nionyeshe anavyokuogesha? Anaingia chumbani kwako? Kama wanakaa chumba kimoja, mkilala na flani inakuaje, anakugusa?

(3) Ulipoenda sehemu flani nani alikua rafiki yako? Mkiwa huko nani alikua anawanunulia zawadi, sisi wakati tunasomja ilikua hivi na vile, Mwalimu wetu alikua anatupenda… vipi shuleni ni Mwalimu gani anakupenda….”

Ongea na mwanao kama rafiki, acha kumhoji maswali kama polis, kwa maana hiyo usimuulize maswali mengi kwa siku moja, mimi nimeandika hapa ili kukushtua tu, ila leo unaweza kumuuliza swali moja, kwa uchangamfu na ukaonyesha kuwa hata hujakasirika bila kujali majibu yake, kesho, ukakaa baada ya wiki lengo ni ili mtoto azoee na asiwe na uoga.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA