MCHUMBA WANBU ANATAKA KUNIACHA MWEZI MMOJA KABLA YA HARUSI?



iddimakengo 
Ndoa yangu ni mwezi wa pili kaka, niko kwenye mahusiano huu ni mwaka wa nne, sijawahi kumsaliti mpenzi wangu wala kuhisi kufanya hivyo. Ila Kaka kuna tatizo moja na sijui nafanya nini, kuna Kaka mmoja kwenye mitandao tumezoeana, sijawahi kuonana naye wala hata kuongea naye ila huwa napenda kucomennt kwenye picha zake na kila kitu anachopost.

Yeye pia hufanya hivyo kwenye ukurasa wangu, kwasababu hiyo tumejikuta tunakua marafiki na mara nyingi tunakua tukichart mambo ya kawaida. Anajua nina mchumba wangu na tumezoeana kiasi kwamba mambo yangu na mchumba wangu namuambia, mwezi uliopita nilimuambia kuwa ninaolewa.

Alinipongeza na kuniambia kuwa atanipa mchango kwenye harusi yangu, basi kwa mara ya kwanza akaniomba namba ya simu nikampa akanitumia laki tatu. Baada ya kunitumia tukawa tunachart tu tunajuliana hali na vitu kama hivyo. Mimi niko Dar na yeye anaishi Arusha, wili iliyopita alinaimbia kuwa anakuja Dar na akipata muda basi atataka kuja kuniona kabla ya ndoa basi nilimuaomba sawa kama rafiki.

Kweli alikuja na weekend hii aliniambia sehemu ambapo kashukia basi mimi nikaenda kuonana naye. Alishukia hoteli kubwa tu, nilimuaga mchumba wangu kuwa naenda kuonana na rafiki yangu, kwakua najua wanaume walivyo na wivu sikumuambia kuwa ni rafiki wa kiume. Nilienda kweli aliposhukia, sikuingia chumbani, nilienda kukutana naye sehemu ya wazi tukaongea mpaka jioni.

Wakati nipo kule kwa bahati mbaya simu yangu ilizima chaji, nilikaa mpaka kwenye saa mbili hivi ndiyo yule Kaka kwakua alikua na gari alinirudisha nyumbani. Kumbe kipindi chote hicho simu yangu haina chaji mchumba wangu alikua akinitafuta kwenye simu, nilifika nyumbani yule Kaka alinishusha na kuondoka, wakati huohuo ananishusha mchumba wangu naye ndiyo alikua anaingia.


Hakuongea kitu alichukua tu simu yangu na kuondoka nayo. Hanaga kawaida ya kupekua simu yangu na kwakua nilikua sifanyi kitu kibaya huwa sifutagi meseji. Sikujua hata kama anajua password yangu, alienda na kufungua simu yangu, akaona namna nilivyokua na wasiliana na yule kaka kama rafiki tu, hakukua na kitu kibaya, alione pesa aliyonitumia na jinsi alivyotaka tukutane.

Jumapili alikuja kwangu na kuniambia kuwa tumemalizana akiamini kuwa nilikua nimeenda kufanya mapenzi na yule Kaka. Nilijaribu kumuelewesha kuwa yule mtu ni rafiki tu lakini hakuelewa, aliniambia kama tumebakiza mwezi mmoja kabla ya ndoa lakini namsaliti hawezi kuingia na mimi kwenye ndoa. Kaka nimeomba msamaha mpaka nimechoka, huyo Kaka ni rafiki tu ambeye tumezoeana kwenye mitandao na alitaka kuonana tu na mimi.

Nilienda hotelini kwake kweli lakini sikuingia chumbani, nimemuomba hata twende kwenye ile hotali kwani ni hoteli kubwa kuna kamera tuombe kuziona ila hanielewi. Anachoamini nikuwa ni mpenzi wangu na kwakua tulikua tunataniana taniana kwenye meseji basi anaamini kuwa natembea naye. Kaka si kwamba hata nilikua namuambia nampenda au alinitongoza.

Kaka wa watu hajawhai kunitongoza ni ile tu napost picha ananisifia inbox basi, nisaidie, sijamuambia mtu yoyote kwani naona aibu. Kila kitu kishakamilika, vikao na kila kitu ila mwanaume ananiambia ananipa muda ili nitafute sababu ya kuwaambia wazazi wangu lakini yeye hawezi kuendelea na ndoa, nisipowaambia mimi atawaambia yeye na kuwaambia na sababu ya kuniacha, nisaidie kaka nifanye nini?

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA