MUME WANGU ANATAKA TUUZE NYUMBA AMBAYO ALINIKUTA NAYO ILI TUJENGE NYINGINE!




Mimi ni mwanamke wa miaka 35, nimeolewa na Mungu kanijalia mtoto mmoja na sasa hivi nina ujauzito wa mtoto wa pili. Tatizo nililonalo ni huyu mume wangu, kabla ya kuolewa naye niliolewa na mwanaume mwingine ambaye ndiyo nilizaa naye mtoto wangu wa kwanza, kwa bahati mbaya yule mwanaume alifariki dunia hivyo kuniacha mimi na mtoto. Nashukuru kipindi hicho mimi na huyo mwanaume tuliweza kujenga.

Ni mwanaume ambaye tulishirikiana kwa kila kitu hivyo hata katika kujenga tulijenga pamoja, alipofariki ndugu zake hawakudai chochote kwani kila mmoja ana maisha yake. Niliamua kutokujiingiza katika mahusiano kwa miaka mitatu mpaka nilipokutana na huyu mume wangu wa sasa. Mimi nafanya kazi nayeye anafanya kazi, yuko vizuri anampenda mwanangu na anahudumia kwa kila kitu.

Tatizo nikuwa anataka kusimamia kila kitu, hata vile ambavyo nilichuma na mwanaume wangu wa kwanza, vile ambavyo alinikuta navyo, alinikuta na gari sasa analitumia kama lake, hilo mimi sijali kwani ni mambo ya anasa tu. Alinikuta na biashara lakinia ansimamia yeye, anafanya maamuzi mengine ambayo hata siyaelewi, nikiongea anasema namnyanyasia vitu vyangu. Hata biashara sikujali bali kuna suala la nyumba ambayo nilijenga na mume wangu wa zamani.

Ananiambia hiyo nyumba haiko sehemu nzuri hivyo nivyema tukaiuza na kujenga nyingine, analazimishia sana tuiuze na kuna wakati alipata hata mteja kabisa. Nimekua nikimkatalia lakiniananuna na kuniambia simsikilizi, anasema namdharau kwakua najihisi kwamba nina pesa. Nyumba imekua haina amani kwasababu hiyo, anakasirika vitu ambavyo havieleweki, kusema kweli nampenda, lakini nahofia kama tukiiuza tutajenga nyingine kweli, naomba mawazo yenu kwani ndoa bado naitaka na nyumba naogopa kuuza.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA