Dada mmoja aliniambia, ninatamani sana kufanya biashara lakini kila mtu ninayemuomba ushauri ananiambia biashara ni ngumu na kwa namna nilivyo sitaweza. Watu wananiambia kua siwezi kuhangaika kutafuta mzigo, Baba yangu ananiambia ni bora kutafuta kazi ya kuajiriwa kwani mimi ni mpole sana hivyo ninaweza kutapeliwa na kuishia kulilia. Mpenzi wangu ananiambia atanipa kila kitu hivyo sina haja ya kujisumbua kwani biashara ni ngumu sitaweza.
Lakini kaka mimi nina hamu sana ya kufanya biashara ila najiona kama siwezi kwani hata Mama yangu mzazi ananiambia kua siwezi kufanya biashara. Nilimuangalia na kushangaa, kwanza hakuna mtu ambaye kazaliwa ili kufanya biashara na suala la mafanikio halijalishi kama unalia au hulii, kama umwembamba au mnene, kama u mwanamke au mwanaume ananiambia anataka kuchukua mkopo ili ampe mchumba wake na wafungue biashara kwa pamoja mchumba wake aisimamie kwani yeye hawezi kusimamia.
Nilimuambia asubiri nitampa jibu, baada ya wiki moja nilimtafuta na kumuambia, unaonekana una umwa, kwa namna unavyoonekana utakua na Malaria, lakini inawezekana una UTI na aleji, aslinishangaa sana na kunaimbia yeye yuko sawa na wala hana tatizo lolote. Nilizidi kumkazania kua anaumwa na anahitaji kwenda kupima alikataa na mimi nikamkazania akapime kwani ni mgonjwa. Nilimuambia kwa kumuangalia tu najua anaumwa asipokua makini Malaria itapanda kichwani na anaweza kufa.
