MAPENZI NI BASI LA SAFARI KILA MMOJA NAULI YAKE ITAAMUA ITAMFIKISHA WAPI

Mwanaume, Ukiishi kwa kuamini kuwa pesa ndio kila kitu kwa wanawake, basi jiandae kuchunwa kila siku. Na ukiishi kwa kuamini kuwa mapenzi hayahitaji pesa, basi jiandae kuachwa na kila mwanamke.
Siku zote mwanaume mjinga hawezi kumuoa malaya bali atavuruga furaha ya familia yake kwa sababu ya malaya.
Ndoto kuu ya kila mwanaume nikuwa na mwanamke msikivu, mwenye heshima na mtiifu. Jambo la ajabu huwa ni pale mume anapotaka mke wake amheshimu, amsikilize na amtii wakati yeye hawezi kumsikiliza mke wake wala kumtii.
Hii ni sawa na kujitazama kwenye kioo ukiwa umenuna huku ukitaraji mtazamo wa taswira yako kwenye kioo icheke.
Na nyinyi dadazangu Waafrika siwezi nikawaacha kitupu, sababu mara nyingi mtu anakuacha kwa mbwembwe nyingi (Anakusaliti) ila baada ya muda flani. Miezi, mwaka au miaka.... Mtu huyo huyo hurudi tena kwako na kuomba mrudiane.
Kwa asilimilia kubwa nimeshuhudia watu wakipumbazika akili kuwa "KAJIRUDI, sasa itakuwa amegundua kosa lake na ananipenda" anasahau kama anakumbatia bomu la machozi hivyo anaamua kurudiana naye.
Mwisho anajikuta anachakazwa tena nakuishia kuuumizwa kama mwanzo.... Hapa ndio unakuta binti akiyachukia MAPENZI daima.
Dada kama umeachwa na mtu kuwa na msimamo usikubali kuyumbishwa yumbishwa sababu huenda ikawa huko alikotoka amepachikwa mzigo wa gonjwa usio kuwa na TIBA, sasa anataka umpunguzie uzito wa sononeko la moyo wake kwa kujinadi kuwa munakufa wote.
Dada, usidhubutu kuhisi sex ndio itafanya mwanaume asikuache wala usihi kubebeshwa mimba ndio kutafanya uolewe na mwanaume unaempenda. Unapompenda mtu asiekupenda hata ukampa mwili wako atakugeuza chombo cha kutolea hamu yake tu.
Nakueleza yote haya kwa sababu mabinti wengi sasa hivi hawajui kuwa kutongozwa sio kuolewa.
Amini nakuambia, usipokuwa makini makinika. Acha tabia ya kumkataa mtu sahihi kwako kwa kisingizio cha mtu aliekukosea. Unajipotezea nafasi mwenyewe alafu utabaki ukisaga meno na kulia huku ukienda kula harusini mwa wenzio tu.
Yazingatie sana yote niliyokuambia, shauri yako likikupata utanikumbuka tu.


Usijisumbue kwenda kwa waganga eti kisa upate mume wakati mganga mwenyewe hata yeye aliachwa na mke au mumewe.







*UKIPENDWA PENDA UTAKUJA PENDA USIPENDWE.