MWANAUME ANAPOSEMA NAMUACHA TARATIBU ANAMAANISHA NACHEPUKA KWA UHURU!




Sijui kama kuna mwanaume ambaye anaweza kuambiwa hivi na mwanamke akavumilia, sijui na sijawahi kukutana naye, kama upo daa.. nimekuvulia kofia, Kitabu changu kijacho nitakupa bure. Lakini wadada ndiyo wanaongozwa kudanganywa “Ninamuacha taratibu!” Yaani umekutana na mwanaume, mwanzo alikuambia hajaoa au hana mapenzi ukaja kugundua baadaye baada ya kukuta meseji au mwanamke ni msumbufu hivyo anapigiwa mara kwa mara ukashtuka.

Mwingine alikuambia kabisa kuwa nina mpenzi wangu tuko kwenye mchakato wa kuachana lakini tumetoka mbali, au tuna mtoto, tuko kwenye ndoa hivyo namaucha taratibu. “Namuacha taratibu” Huu msatari umetumika mara nyingi kuumiza mabinti. Kwanza kabisa ni upuuzi tu, hakuna kitu kama hicho, katika mapenzi hakuna kuachana taratibu. Mwanaume anapokuambua namuacha mke wangu, mpenzi wangu, rafiki yangu, au hata jirani yangu taratibu ni njia nyingine ya kukuambia nachepuka kwa uhuru.

Atajifanya huyo mwanamke mwingine ni king’ng’anizi lakini ukiangalia anajibu SMS vizuri, akipigiwa anapokea na kujichekesha. Anakuambia namuacha taratibu ili siku ukimfumania, siku ukikuta kaja kwake, siku ukikuta meseji akuambie “Alikua analazimishia kuja ndiyo maana nikawa sina namna, sitaki kumuumiza namuacha taratibu!” Hakuna kitu kama hicho, mara nyingi mwanaume kama kakuambia hivyo siku na wewe ukipiga simu na yuko na huyo anayeachwa taratibu basi jibu lake kwa huyo mwingine litakua hilohilo.

“Nilitoka naye siku moja sasa amegoma kuniacha ananisumbua, sitaki kumuumiza namuacha taratibu!” Sisemi hatakuoa ila jua anapima na anahalalisha kuchepuka kwake kwa kukuchukulia fala, narudia anakuchukulia fala ndiyo maana anakupa jibu la kifala kama hilo. Kama una akili utamuambia Baba nenda mkamalize kuachana ukija uwe na mimi sitaki kushae, lakini kama wewe ndiyo walewale endelea kuvumilia mwenzako akiachwa taratibu wanaweza kumaliza kuachana 2050.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA