KATAA KUWA TAMBALA LAKE LA DEKI KATA MAWASILIANO NAYE KABISA!






Naomba ushauri wako, kuna Kaka nilikua naye kwenye mahusiano kwa miaka miwili, ghafla akaja kuniambia kuwa hawezi kuendelea kuwa na mimi, ananiambia akiwa na mimi hapati amani hivyo tuachane. Kusema kweli niliumia sana kwani nilikua nampenda na baadhi nya rafiki zangu walikua wanamfahamu.

Nilijaribu kumuomba msamaha kutaka kujua sababu lakini hakununipa. Basi nilikubali kuachika, lakini baada ya kuka akimya kwa miezi mitatu alinitafuta, nilimuuliza sababu akaniambia ameachana na mimi lakini hataki tuache kuwasiliana, kwahiyo akawa ananitafuta, ananipigia simu na tunachart kwa meseji.

Nikimuambia kuhusu kurudiana ananiambia hapana tuwe marafiki tu. Basi nilikubali, lakini kinachoniumiza nikuwa, mimi nikimtafuta au nikimtumia meseji hajibu, anakua mkimya hata wiki, lakini akinitafuta anataka tuchart na anakua mchangamfu kabisa, naomba nisaidie kaka je kuna mapenzi hapa!

JIBU LANGU; Unapoachana na mtu unapaswa kuakata mawasiliano naye, ukiona bado unawasiliana na X wako basi jua bado hujakubali kauchika au hukuwa unampenda kihivyo. Kinachotokea ni hivi, huyo mwanaume ameshakuacha na inawezekana ana mtu wake mwingine lakini anashindwa kukusahau kwakua labda ana upweke flani ambao anataka umsaidie kudili nao.

Huyo mwanaume anakutumia, akiwa na mawazo, akiwa kagombana na mtu wake, akiwa tu bored anataka mtu wa kuongea na wewe anakutafuta kisha akimaliza anakuacha anaendelea na maisha yake. Huyo mwanaume anakufanya Tambala la Deki, unalihitaji kusafishia ndani na kufuta miguu tu lakini halivuki mlangoni, linalala nnje.

Kwamba ukilihitaji tambala la deki kufuta usafi utaingia nalo mpaka ndani, lakini ukishafuta uchafu unalitupa nnje. Hivyo akiwa na shida zake anakutafuta ila zikiisha anakuacha mpaka shida nyingine. Cha kufanya, achana naye, muambie hutaki kuwasiliana naye, akikupigia usipokee, mseji zake hata usisome, endelea na maisha yako kataa kuwa tambala lake la deki!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA