KAMA MWANAUME AKIKUABIA HIVI BASI JUA TAYARI ALISHAKUACHA ZAMANI ANATAFUTA TU SABABU!




Dada zangu huyo mwanaume wako anaweza asiwe mume wako, anaweza asikuoe kwakupata mtu mwingine lakini asikuoe kwakua Mungu hakupanga labda akatangulia. Kwa maana hiyo basi hakikisha vitu ambavyo unafanya naye leo havina athari kwa mume wako mtarajiwa, kuna mambo ambayo ukishayafanya hayabadiliki tena na inawezekana yeye kwa sasa akaona kama ni kawaida lakini huyo mwingine asione kama ni kawaida.

Kila kitu unachokifanya katika mapenzi fanya kwakua unapenda lakini si kwakua mwanaume anapenda, kwa mfano kama unafanya mapanzi kinyume na maumbile fanya kwakua unapenda na utapambana na Mungu wako au hata ukiachwa lakini ulienjoy, usifanye kwakua mwanaume kakuambia anapenda na usipofanya anakuacha kwani atakuja kukuacha na utaishi kwa majuto kila siku. Kama unapenda kuchora tattoo sehemu za siri chora kwakua unapenda na una enjoy na si kwakua mwanaume anapenda na unataka umshike.

Kama unapenda kupiga picha za uchi piga nyingi uwezavyo kwakua unapenda na unaenjoy kujiona uchi na si kwakua mwanaume anapenda na anakuambia kua usipopiga basi anakuacha, mwanaume anayekuambia usipofanya kitu flani anakuacha basi jua alishakuacha muda mrefu anatafuta sababu tu ya kijinga ili akuache. Narudia ukiona mwanaume anakuambia kama hutafanya kitu flani nakuacha basi jua kua hakupendi, narudia hakupendi, anachofanya ni kukupima, hivyo anakuambia kitu cha kijinga akitegemea kua hutafanya.

Lakini kwakua labda unampenda sana na unajidanganya kua labda yeye ndiyo alivyo basi unamfanyia kumridhisha lakini ukweli nikua hakutaki ndiyo maana anakuambia mambo ya kijinga jinga ambayo anajua mwanamke mwenye heshima zake ambaye anaweza kuwa mke wa mtu atakataa ili akuache. Hivyo sikuambii usifanye ujinga, hapana ni maisha yako lakini usifanye kwaajili ya mwanaume eti unaogopa kuachwa, hapana wanaume wenye tabia hizo ndiyo walivyo na atakuacha tu!

Kama unajua kabisa roho yako haitaki, unajua kabisa kua kama ukiachika basi utaumia kwa kufanya kile kitu acha kwani utaachika tu hata ukilifanya. Lakini jua kua mambo haya hayarudi nyuma, tattoo haifutiki, picha za uchi hazifutiki na mapenzi kinyumEster haiishi!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA