KAMA KILA SIKU UNALALAMIKA HUPATI HUPATI WANAUME SIRIASI BASI SOMA HAPA!




Hili ni lalamiko la wanawake wengi, hapa iwe ulikua unatembea na mume wa mtu au la. Unapoachana na mtu uliyedumu naye kwa muda mrefu, au unapomaliza utoto wanwake wengi huanza kutafuta wanaume ambao ni siriasi.

Saasa labda niwaambie tu kitu kimoja, hakuna wanaume wa namna hiyo. Yaani mwanaume anakutongoza siku ya kwanza anaonyesha yuko siriasi anataka kuoa huyo ni muongo.

Lengo la kwanza la mwanaume la kutongoza kwa waliowengi ni kufanya mapenzi basi. Ndoa na usiriasi huja baadaye na si baada ya siku mbili tatu. Hivyo usiadhani kwakua kakuambia nataka kuoa, kakuambia kachoka kudanga na hivyo anamaanisha.

Wanaume wengi siku hizi wanajua kua wadada wengi wanapenda ndoa hivyo wewe ukishamlalamikia kuwaumeumizwa sijui unataka mtu siriasi nayeye atakuambia anataka kuoa. Wengine ni washenzi zaidi ataenda hata kukutambulisha kwa dada yake na shangazi au marafiki.

Lakini lengo ni lilelile kukutumia basi. Sasa hembu acha kutafuta mwanaume siariasi kwani hayupo, tafuta mwanaume anayekufaa. Hapa nikimaanisha kuwa angalia muonekano wake je ndiyo unaoutaka, angalia namna anavyokjali, si kutoa hela hapana anavyojali hiasia zako.

Angalia namna navyokuheshimu kama mwanamke na mambo megine ya nnje. Kama yote hayo ni sawa basi furahia mahusiano, usisukume ajenda ya ndoa au kuwa siriasi mapema. Iko hivi miezi miwili ya kwanza uliyopo na mwanaume wako mpya anakua bado hajamalizana hata na mpenzi wake wa zamani.

Najua unashangaa lakini usidhani kua mwanaume akikutongoza basi alikua single hapana ana mtu tayari hata kama si siariasi lakini yupo. Hivyo wewe angalia je huyu tutaendana kama mtaendana basi huo usiriasi utapatikana katikati mkishasomana tabia.

Lakini kama ukitaka siku ya kwanza awe siariasi, aanze kukujali siku ya pili, akutreat kama galfriend siku ya nne basi utatafuta sana na hutampata.

Utajiona kama huna bahati labda unamikosi kumbwa una haraka tu, punguza spidi utaona namna hao ambao hawako siriasi wakikuona unajielewa atakua siriasi.

Ondoa presha ya kutaka kuolewa na kutaka kupata mwanaume ambaye yuko siriasi.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA