Kuchukulia Poa Mambo Madogomadogo/Unalimbikiza Mateso.

 





Watu wengi hudhani kuwa ndoa au mahusiano huvunjika kwakua wahusika wanafanyiana mambo mabaya makubwa, hapana, mpaka kuvunjika kwa mahusiano hasa kwa upande wa kina Dada wanakua wamevumilia mengi. Kwamba mwanaume haanzi tu na kukupiga bali huanza na manyanyaso kidogo kdogo mapaka kufikia huko.


Sasa watu wengi amabo huumizwa sana wanatabia ya kuvumilia mambo madogomadogo, mtu anaonyesha dalili flani badala ya kuongea unanyamaza na kuchukulia poa, tuseme anakudharau unachukulia poa, anakukashifu unaishia kulalamika basi, huchukui hatua, sasa baada ya muda unakuta umelimbikiza mambo mengi moyoni, unaanza kuona kawaida wewe kufanyiwa hivyo.
Tena unaona mhusika anatabia ka a za yule lakini bado unavumilia na mtakuja kauchana tena kwakua hujarekebisha awali na utalia tena. Sasa hapa nini chakufanya, cha kufanya nikuwa hembu kama mambo hayaendi sawa kaa uzungumze naye mapema,acha kulalamika, hapana unapolalamika ataona ni tabia yako kulalamika, ongea naye muambie hili hapana hili sawa.

Kwamba awali kabisa ukiona anaanza tabia flani huitaki basi muambie hii sitaki na asipobadilika ondoka. Achana na ule msaemo nitaachana na wangapi, hata kama ni mia lakini kuandelea kubaki kila siku unalia haikusaidii kwani usipomuacha wewe atakuacha yeye kwakua hakuna mtu anayependa mtu anayevumilia ujinga. Kama huamini hembu muangalie X wako, si ulivumilia sasa mbona kakuacha?

Iko hivi unapovumilia mateso muda mrefu basi unakosa furaha, unapokosa furaha basi unaboa, hakuna mtu anapenda kuishi na mtu aliyenuna kila siku hata kama yeye ndiyo anamsababishia kununa. Sasa atafanya mambo mawili, kwanza anaweza kutafuta mwingine, sehemu ya kwenda kuongea na kucheka au atakuacha na kutafuta mwingine kabisa, nadhani umejifunza kitu hapa.

Mwisho nimalizie kwa kusema kama uko katika mahusiano ya aina yoyote ambayo unaona huna furaha, kama ni mwanaume au mwanamke basi soma shemu ya nne ya Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” Jifunze namna ya kujipenda, namna ya kuwa na furaha bila kujali mtu mwingine. Furaha yako haipaswi kuwa hisani ya mtu, inapaswa ikutegemee wewe na isimtegemee mtu maelezo ya Kitabu pitia post nyingine.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA