KWANINI WANA NDOA WA SASA WANAAMINI ZAIDI MAPENZI YA NJE YA NDOA KULIKO YALIYOKO NDANI YA NDOA🤔


Kwanza fahamu jambo hili;-
👉🏼 NDOA NYINGI KWA SASA ZINAPATIKANA BAADA YA MAUMIVU YA MAPENZI.
Wengi wanaanzia kwenye kutumiana ki mwili👙 na kuachana na hapo ndipo mtu mke ama mme kutafuta Mwingine yeyote ambaye ataendana na hitaji lake bila kupima MOYO wake na hapo ndipo wakiishi japo kwa mwezi mmoja kila mmoja anaanza kujutia na kufikiria ALIKITOKA KULIKUWA BORA ZAIDI ndipo roho ya ubinafsi hutenda kazi.
Kinacho hangaisha NDOA nyingi ni MUDA WA KUWA PAMOJA na saa zingine ile hali ya kuhitajiana ki mwili, Majukumu mengi ni GANZI YA MAPENZI sio kwa Wanaume tu hata kwa WANAWAKE.
Ndo maana wana ndoa wanakimbilia kwa WANAUME na WANAWAKE wasio na majukumu japo hawajui kuwa na wewe huyo unae amini hana majukumu tayari wewe unakuwa jukumu lake maana hakosi kuwa na AMPENDAYE maana yake wewe UTAGHARAMIA UWEPO WA ULIYEMKUTA😂
Kama wana ndoa wakipata muda wa kukaa pamoja, Kuhitajiana ki Mwili na Mengine yanayoendana na KUIMARISHA NDOA siamini katika kuchepuka💯
Muda Mwingine wana ndoa wanahadaika na PENZI TAMU LA WIZI kwani hata anayedokoa mboga kabla haijawekwa mezani anaujua utamu kuliko ikiwa mezani😂
Usaliti ni moja ya MAUAJI YA POLEPOLE wengi wanaangukia maradhi kwa kuyawaza MAHUSIANO NA NDOA zao, Tatizo haliibuki mara moja ila huja taratibu mwisho ni MADHARA.
Bakia na UMPENDAYE KWA MOYO haijalishi ni MAPITO gani unapitia ila lililo la THAMANI NI ULINZI WA NAFSI 💯
Image may contain: 1 person, sleeping

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA