USHAURI KUHUSIANA NA WIVU ULIOPITILIZA



💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚Wivu ni hisia zenye ncha mbili zenye makali sehemu zote, na ni miongoni mwa vitu muhimu katika kusukuma damu mpya katika uhusiano wa wanandoa. Lakini wivu huo unapopitiliza kiwango chake cha kawaida na cha asili hugeuka kuwa tishio dhidi ya ndoa na familia yote. Hivyo mwanandoa anapaswa kuitambua hatari ya wivu uliopitiliza na ajifunze namna ya kuyatuliza mambo iwapo atahisi kuwa wivu unatishia mustakbali wa ndoa yake bila sababu ya msingi.
Famasia yako ya Ndoa Maridhawa inakuletea ushauri utakaokusaidia kukabiliana na jinamizi la wivu wako kwa wakati maalum na njia za kuishinda changamoto hiyo:
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
SUBIRI NA UZUNGUMZE NA MUMEO KABLA YA KUTAMALAKIWA NA WIVU:
Unatakiwa kusubiri kidogo na ulifikirie jambo husika kabla hujakimbilia kuchukua hatua za wivu. Hivyo usimshambulie mumeo kwa lugha kali, bali zungumza naye kuhusu jambo hilo kwa namna isiyokuwa ya moja kwa moja kiasi kwamba ataijua sababu yaw ewe kuhisi wivu wako ili asirudio jambo hilo hapo baadaye.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
ZISIKILIZE SABABU NA HOJA ZAKE:
Hutakiwi kumshambulia mumeo kabla ya kufanya mazungumzo. Huwenda umemhukumu kimakosa au hajakusudia kufanya aliyoyafanya. Hivyo, mpatie fursa ya kuelezea hoja zake kwanza kisha ndo umhukumu. Ukimpa nafasi hiyo atakuwa na fursa ya kujitetea na kuelezea sababu zake kwa uhuru, na hilo litakuepusha kuingia kwenye mtego wa kuongeza kosa juu ya kosa ambalo linaweza kusababisha matatizo hapo baadaye.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
TUMIA SILAHA YA UTULIVU
Epuka mlipuko… mlipuko hautamfanya akusikilize, bali unaweza kuongeza moto zaidi. Zungumza na mumeo kwa utulivu kuhusu jambo husika, huwenda mazungumzo yakifanyika kwa mlipuko yakaongeza matatizo zaidi. Hivyo, ili mazungumzo yafanyike kwa njia sahihi na kutatua tatizo, zungumzeni kwa utulivu sana na kila mmoja aheshimu maoni ya mwenzake ili kutoibua matatizo zaidi. Ili kujizoesha kuwa mtulivu wakati wa mazungumzo yoyote yale unaweza kufanya mazoezi ya Yoga na pia TAFAKURI ili kuondokana na mizigo ya HISIA HASI na badala yake uzibadilishe kuwa HISIA CHANYA.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
EPUKA HISIA ZA WIVU KATIKA WAKATI MUAFAKA:
Unapokuwa katika eneo fulani na ukahisi wivu uliopitiliza kutokana na mumeo kuwa karibu au jirani na wanawake, basi ondoka eneo hilo. Ukihisi kuwa hali yako inaweza kubadilika na kuwa mbaya zaidi, basi jaribu kuwa busy na mambo mengine. Kadhalika unaweza kuamua kwenda kutembea na watoto wake au kutazama filamu nzuri au kufanya mazoezi au kutoka na marafiki zako.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
EPUKA UHAFIDHINA:
Upendo ni hisia tamu na nzuri ambazo mtu huwa nazo kwa ajili ya mwenza wake, lakini upendo huo ukizidi kiwango na ukawa upendo wa kumdhibiti na kumtawala, hatokuwa na furaha Abadan. Hivyo, usimgeuze mumeo kuwa mwanasesere unayemdhibiti. Yaani usimlazimishe mumeo muda wote awe mtu wa kutoka kazini na kukaa nyumbani tu, bali mfanye awe mwanajamii. Mhamasishe aende mazoezini, mpe fursa ya kutoka kwenda kwa jamii.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
JIAMINI:
Wivu uliopitiliza unatokana na sababu kubwa moja, nayo ni kutojiamini… kukosa confidence ni tatizo kubwa sana ambalo linaenda kukutesa mpaka kwenye tendo la Ndoa. Tambua kuwa mumeo ndiye aliyekuchagua wewe bila kulazimishwa. Hivyo, anakupenda kwa moyo wake wote hata kama ana mambo mengi yanayomshughulisha mwishowe atarejea kwako na kufurahia mahabba yako.
💚💚💚💚💚💚💚💚💚💚
ACHA UJASUSI:
Jukumu lako namba moja ni KUINGIA KWENYE MOYO WA MUMEO. Kila siku unatakiwa kuwa katika safari ya kuingia kwenye moyo wake. Acha kazi nyingine zote ujikite kwenye jukumu hilo. Ndiyo maana kila siku huwa ninasema kuwa kwenye ndoa hakuna ajira ya ujasusi, kwenye ndoa kuna ajira ya kuingia kwenye moyo wa mtu. Ajira ya ujasusi inapatikana polisi na idara ya usalama wa taifa. Acha kujitia presha kwa ujasusi. Hiyo ni sumu mbaya, utajiumiza bure.

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA