NINA MIEZI 6 TU ILA NAONA KAMA NISHAMCHOKA MKE WANGU!






Mimi nimeoa ndoa yangu ina miezi sita sasa lakini nashindwa ni namna gani naweza kuishi na huyu mwanamke. Mimi nafanya kazi Benki, kutokana na cheo changu kwa kawaida natoka kazini saa mbili na wkaati mwingine mpaka saa nne usiku nipo kazini.

Mke wangu anajua kazi yangu na anajua kuwa sipo na wanawake wengine. Lakini shida mke wangu ni mtu wa kulalamika sana, yaani anapenda kuchart na mimi kila siku, yeye ni mfanyakazi wa serikali, kutokana na nafasi yake anakua hayuko bize kabisa.

Kila wkaati anapenda kuchart na mimi,a kiniona online tu atatuma meseji hata kumi nisipojibu atapiga nisipopokea atatuma meseji zaidi ya kumi kulalamika. Nikirudi nyumbani ndiyo shida, kila siku kanuna, unakuta unarudi nyumbani, unamawazo ya kazi naye anaongea mpaka unakasirika.

Najaribu kumuelewesha lakini kila dakika analalamika kuwa mimi namdharau, simpendi, anaapiga simu nyumbani kila siku mpaka nimeanza kumchoka. Mimi nakunywa pombe ila kutokana na kazi yangu siku za kazi nakjizuia, lakini tangu nimeanza kuishi na mke wangu nimejikuta kila nikitoka kazini napiga hata mzinga wa konyagi ili tu nikirudi nimezima nisimsikilize mke wangu.

Nimekunywa pombe ila naona kama itaniharibai na kazi kwani naamka nikiwa nimechoka, naomba unisaidie ni namna gani naishi na mwanamke wa namna hii. Analalamika mpaka kuna wakati niko ofisini natamani kumpigia mke wangu simu ili kuondoa mawazo nashindwa.

Kabla ya mke wangu nilikua na mahusiano na Dada mmoja tukashindwana kwasababu ya dini. Huwezi amini kila nikikorogishana na mke wangu nataamni kumtafuta, nilishachart naye mara kama tatu hivi nakua na rafaja kwania ananielewa na si mtu wa kulalamika.

Baada ya kuanza kukusoma nimeacha kuwaisliana naye kwani nimeona kuwa si sawa. Ila naomba msaada wako, ndoa ina miezi sita, nampenda sana mke wangu, kipindi cha mahusiano alikua anajua kazi yangu.

Hakua akilalamika kama sasa, alikua ni faraja yangu, nikiitoka kazini nampigia tunaongea nafurahi, nikiwa na stress naejoy kuongea naye, nikimuambia niko bize ananielewa, nisaidie nifanye nini sasa, sitaki kuchepuka wala sitaki kumuacha mke wangu ila ndoa nimeichoka!

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA

DOWNLOAD APP YETU GOOGLE PLAY BONYEZA HAPA