SHOGA YANGU ANAMLOGA MUME WAKE NIFANYE NINI KUMSAIDIA SHEM?
Kaka usije ukanichamba maana hujui mambo ninayopitia. Iko hivi mimi niliolewa, lakini mume wangu alinitelekeza kipindi sina kazi, so rafiki yangu akanichukua wakati nikiwa na ujauzito hivyo nikaenda kuishi kwake, nikajifungua na ikawa hivyo.
Katika kipindi niko kwake kweli nilimpenda mume wake, mume wake ni ile aina ya wanaume ambao wanajali, anahudumia, yaani sijui nikuambieje Kaka, kwanza ni mzuri and sioni kama anaendana na huyo rafiki yangu. yaani rafiki yangu ni mzuri ila ni mcharuko flani hivi, sio kama ni malaya halana ila anaongea na wanaume hivyo yani.
Mwaka jana rafiki yangu alicheat, alichepuka na X wake, so niliona kama ni fursa ya kuwaharibia basi nikavujisha meseji mume wake akaziona, ilikua ni ugomvi mkubwa sana mwanaume akamfukuza rafiki yangu so na mimi ikabidi niondoke. But cha ajabu mwanaume alimsamehe, hapo ndipo nilihisi kuna kitu.
Basi nikaamua kwenda kwa mtaalamu akaniambia kuwa huyo rafiki yangu kuna kitu kamuwekea mume wake, yaani kama kamfunga flani. Mimi namimi nikachukua dawa, basi kwakua hakuna aliyejua mwanzoni kama mimi ndiyo nilivujisha meseji kwani nilijifanya kama mimi ndiyo mwanamke wa huo mchepuko wa shoga yangu.
Nikatafuta namba ya mtu mwingine na kumtumia mumewe mseji na mapicha ya mke wake basi tuliendelea kuwa marafiki. Ila hakuachwa, nimejua shoga yangu anamloga mume wake. Kusema kweli nampenda huyo Kaka si kimapenzi lakini najua rafiki yangu anamloga, nataka kumpa dawa ili kumfungua ila sijui nitafanyaje.
Kaka simtaki shemeji yangu kimapenzi ila namuonea huruma kwani wewe unajua hakuna mwanaume ambaye anaweza kumfumania mke wake na kumuacha. Nataka kurudi ile nyumba ila sasa hivi sina sababu kwani shem alinitafutia kazi, nisaidie nifanye nini, au niache kazi nidanganye nimefukuzwa ili wanichukue tena, nisaidie Kaka ili nimsaidie mwanaume mwenzako!