UKIONA UKO HIVI JUA BADO HUJAMSAHAU X WAKO!
Ukiona unatumia muda mwingi kumjibu X wako kuwa sasa hivi upo kwenye mahusiano mengine, mara sijui una furaha, mara unakumbushia jinsi alivyokuumiza na mambo mabo kibao na kumringishia mahusiano yako mapya basi jua kuwa hujamsahau huyo X wako.
Narudia ni hujamsahau, ulikua bado unamkumbuka na umepata ka ahueni kuwa kumbe bado anakutafuta. Mwanaume au mwanamke ukishaachana naye na una furaha huna haja ya kumjibu meseji yake. Yaani hata ukisikia kafa kwaajili yako mshipa wa uzazi haushtuki.
Huna haja ya kumuelezea unavyodekekezwa na ulivyo na furaha, huna haja ya kumuambia kuhusu mahusiano yako mapya. Akikutafuta huna hata haja ya kumuambia una mtu! Inamaana usingekua na mtu ungemkubali? Sana sana ni kumuambia sikutaki tena akizidisha kelele unamuambia Kajambe mbele kisha anakula Block!
Ila kama ukijiona unajibu meseji magazeti kujielezea, basi jua bado unampenda na kama akikomaa vizuri akaomba muonane mnarudiana bila kujijua. Kwa maana hiyo, X wako akikutafuta muambie sikutaki, huna haja ya kumuambia una mtu, una furaha, umeoa/kuolewa, muambie sikutaki kisha block!