NAMNA YA KUISHI NA MWANAUME AMBAYE ANAPENDA KUKUDHALILISHA KWA MATUSI
Amekua ni mume wako, mnaishi pamoja au mko kwenye mahusiano. Kila unapokosea au wakati mwingine hata kama kosa ni lake lakini hawezi kuongea na wewe kistaarabu. Atatafuta namna yoyote ya kukutukana na kukudhalilisha. Matusi yake makubwa ni ‘huna akili, sijui kwanini nimekuoa, mbaya, unanuka, mjinga, wewe si wa hadhi yangu na vitu kama hivyo.
Kuishi na mwanaume wa namna hii ni changamoto kwani anavyoongea kuna siku utakua teja na kuamini kuwa labda ni kweli huna akili, umbaya, umjinga na unanuka kweli. Kuna wakati unatamani kuondoka na kumuacha lakini unashindwa labda kwasababu ya watoto, wewe mwenyewe unampenda tu au sababu yoyote ile. Kama huwezi kumuacha mwanaume wa namna hii basi mbinu zifuatazo zitakusaidia kuishi naye.
(1) Jua kwanini anapenda kutukana na kukudhalilisha; Ni ngumu sana kwa mwanaume anayejielewa, anayejiamini kumdhalilisha mwanamke wake kwa matusi ya nguoni hasa mbele za watu. Hata kama mwanamke ni kichomi, ana kisirani anake ataongea naye kistaarabu, atakasirika na kufoka kidogo ila si kumtukana mbele za watu, watoto au matusi ya nguoni. Kuna sababu nyingi wanaume wanafanya hivi ila kubwa ni kutokujuamini.
Anahisi umenzidi kitu hivyo anataka kukushusha, labda ana matatizo ya nguvu za kiume, umemzidi elimu, kipato, mwanamke ni mzuri na hajioni kama ni hadhi yake au anamuona mwanamke ana akili ya maisha kuliko yeye. Nyingine ni malezi namna alivyolelewa labda wazazi wake walikua hivyo kwa maana hiyo chunguza jua sababu kwanini anapenda kukudhalilisha.
(3) Usipende kujibishana naye mbele za watu; Wanaume wa namna hii wanajiaminisha kuwa wana hasira sana, kwao kujibiwa na mwanamke ni kama dharau flani hivyo wanapenda kujionyesha mbele za watu kuwa wao ni wababbe, wanajua kila kitu na mwanamke ni kama katakataka flani hivi. Kwa maana hiyo basi, kama una mwanaume wa namna hii hembu acha kubishana naye mbele za watu, akiongea wakati anajaribu kupanda jishushe na omba msamaha hata kama unajua hujakosea.
Muambie nimekuelewa, acha kujaribu kujielezea na kutoa ufafanuzi kwani jinsi unavyozidi kuongea bila kujali kile unachokiongea kwake ataona kama ni dharau, atazidi kupanda na kukudhalilisha. Watu wanapokuja na kumtuliza, kumuambia acha, kumuambia ashushe hasira basi atazidi kukutukana, kukudhalilisha kwani yeye ni kama anaona kuwa yuko sahihi na wewe umekosea. Hivyo kwepa sana kujibishana mbele za watu na mtu wa namna hii.
(4) Mkiwa vizuri ongea naye; Anapokutukana, anapokujibu vibaya, anapofanya kitu cha kukudhalilisha usimjibu hapohapo. Wakati huo anakua na hasira na anaamini kuwa yeye yuko sahihi na anajua kila kitu, kwa maana hiyo, kama ukiongea naye haitasaidia. Subiri kapoa, mko vizuri na hakuna kugombana tena, muambia mume wangu, ulichofanya jana si sawa, ungenielekeza ningekuelewa.
Mara nyingi watu hawa hata wao wanajutia hasira zao wanapotukana na kukudhalilisha mbele za watu hivyo akiwa ametulia itamuuma zaidi kuliko akiwa na hasira kwani wakati uko juu ukimuongelesha atahisi unataka kumpanda kichwani na si kuwa amekosea.
(5) Acha kujaribu kujielezea ili akuelewe, Mpuuze maneno yake kwani hayakuhusu; Kuna wale ambao imekua ni kawaida yao, kila siku ni kukutukana bila sababu, umeshajielezea sana lakini habadiliki, yeye matusi yake ni yale ka kudhalilisha, labda Malaya, labda mjinga, huna akili na vitu kama hivyo. Wanaume wa namna hii wanafanya hivyo kwakua hawajaimini na kuna kitu kinawasumbua.
Matusi yao hayana uhusiano na wewe hivyo hata kama ungekua malaika wangekutukana na hata kama ungekua mbuzi wangekutukana. Kwasababu hiyo ni vyema ukaacha kujielezea, akikuambia mjinga wakati mwingine puuza, acha kujielezea kuwa wewe si mjinga, wakikuambia huna akili, unaweza kuondoka eno husika usitukanwe, ukakaa kimya au kujibu lakini si kwakujielezea au kwakua umeumia bali kwakua na wewe una chakuonge, acha kujielezea na kutaka mtu wa namna hii akuelewe kwani hatakuelewa.

(6) Lalamika lalamika kidogo ahisi kama anakuumiza kumbe unamzuga; Unaweza kuamua kumpuuzia, ukachagua kuwa na furaha yako mwenyewe, shida moja ya wanaume kama hawa nikuwa, ukinyamaza nayo ni shida, anahisi unamdharau, anahisi ushapata mwanaume mwingine. Kwao wanajisikia raha san ausipokua na amani, ukawa mtu wa kulalamika lalamika tu na kulia bila sababu.
Kwa maana hiyo, kama ni mume wako, mwanaume unaishi naye pamoja au unampenda sana huwezi kumuacha. Wakati mwingine lalamika lalamika, akifanya kitu kikakukera jua kafanya makusudi ili ulalamike, basi mpe mlalamiko mmoja, mnuno mmoja ajisikie kanuniwa au anapendwa kwakua kwa akili zao wanaamini kuwa, kama mwanamke asipokununia, akionyesha hajali basi kapata mwanaume mwingine au hakupendi hivyo mpe mnuno bila kuumia.
(7) Badilika kama anayosema ni yakweli kwani kuna watu hawezi kukurekebisha kawaida; Wakati mwingine wanaume kama hawa wanaongea ukweli, kwamba mambo anayokutukana nayo ni ya kweli shida nikua tu hajui namna ya kuyaongea, namna ya kufikisha ujumbe. Kwasababu hizo basi, kama unaona kabisa kuwa mambop anayokulalamikia, anayokutukana ni kweli au unamtengenezea mazingira ajue ni kweli basi badilika.
Kwa mfano anakuita malaya labda ni malaya kweli, una marafiki wengi wanaume, kila saa uko bize na simu na wanaume basi badilika. Anakuita mvivu ila kweli hujigusi, umvivu na umchafu basi badilika. Angalia mapungufu yakoa anyoyaongea badilika kwani shida inakua tu namna ya yeye kufikisha ujumbe ila kwelia anyokuambi ni matatizo yako. Acha kumlaumu yeye tu kuwa anaongea sana bali badilika na acha hayo anayoyalalamikia.